Wazolee
JF-Expert Member
- Sep 1, 2018
- 4,177
- 4,887
Kwa Mujibu wa Taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya Al Jazeera Aprili 6, 2026,
Rais Donald Trump alisema kuwa Marekani ilijaribu kuwapelekea silaha kwa siri waandamanaji wa Iran kupitia wasuluhishi wa Kikurdi, zikiwa zimesalia wiki chache kabla ya vita vya sasa kuanza, hata wakati huo ambao serikali ya Washington ilikuwa kwenye mazungumzo na Tehran.
"Tulituma silaha kwa waandamanaji, nyingi sana," Mtandao wa Fox News ulimkariri Trump akisema hayo, huku akiongeza kuwa rais huyo wa Marekani anaamini Wakurdi walichukua bunduki hizo na kukaa nazo wao wenyewe.
Ripoti za vyombo vya habari, ikiwemo Channel 12 ya Israeli wakati wa maandamano hayo mwezi Januari 2026, pia zilidai kuwa waandamanaji walikuwa wakipewa silaha na "watu wa nje".
Trump alidai pia kuwa, wakati wa maandamano hayo, Iran "iliwachinja" raia takribani 45,000, Fox News iliripoti. Hata hivyo, madai yake hayakuweza kuthibitishwa na vyanzo huru.
Mamlaka za Iran zinasema kuwa watu 3,117 waliuawa katika wiki kadhaa za maandamano hayo, huku zikipinga madai ya Umoja wa Mataifa na makundi ya haki za binadamu kwamba majeshi ya serikali ndiyo yaliyohusika. Maafisa wa Iran wamesema mamia ya maafisa wa polisi waliuawa na mali za serikali ziliharibiwa na waandamanaji hao, ambao waliwabatiza majina ya "wafanya fujo", "wahujumu" na "magaidi". Tangu wakati huo, nchi hiyo imewanyonga watu kadhaa kwa mashtaka ya kushiriki katika maandamano hayo kwa maelekezo ya maadui wa kigeni.
Licha ya kauli hiyo ya Trump, Mohammed Nazif Qaderi, afisa mwandamizi kutoka chama cha upinzani cha Kurdistan Democratic Party of Iran (KDPI) alikana madai hayo hawakupokea Silaha kutoka kwa Trump na kwamba wanaamini kudai haki zetu kwa amani na kistaarabu bila kutumia silaha
Source Trump says US armed Iranian dissidents via Kurds, Kurdish groups deny claim
==========
My take
Hi michezo Marekani huwa wanaicheza katika nchi mbali mbali Ili kuvuruga amani ya nchi husika Kwa kuwatumia wananchi wajinga Ili kazi Yao ya kupora rasilimali iwe rahisi kama walivyo Fanya Libya na Iraq
Ila Kwa Irani waligonga mwamba Trump anakili kuwa kazi imekuwa ngumu Kwa sababu Wakurudi hawakugawa zile siraha Kwa waandamaji
Safi sana Irani Kwa kuwakamata wale waandamanaji vinara na kuwanyonga kama mngewaacha Kuna siku wangeliangamiza taifa lenu Kwa masirahi ya Marekani
Pia Jeshi letu la Tanzania lilifanya kitu sahihi OCT 29 maana mngechelewa tu waandamanaji wangepewa siraha kazi ingekuwa ngumu sana