TSh. 100,000,000 Ni sawa kwa mshindi wa kwanza VPL?

TSh. 100,000,000 Ni sawa kwa mshindi wa kwanza VPL?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Uwekezaji unaofanywa na timu za ligi kuu ya Vodacom unafanana na zawadi ya mshindi wa kwanza inayotolewa?

Tufanye Nini?
 
Uwekezaji wa timu za Uingereza, na anachopata bingwa ni sawa?
Hii ni kote japo kwetu ni kidogo sana.
Timu zinatakiwa kubadilika, kuendeshwa kisasa ili zijiingizie faida.
Ligi ya uingereza na vpl ni mbingu na ardhi, uko uingereza timu inaingiza mapato kupitia, mdhamini mkuu wa timu(kampuni) vifaa vya michezo kama jezi n.k na viingilio lakini pia haki za kurusha matangazo...sisi huku ni tofauti labda
 
Uchumi wa kati. Ukiona hivyo Vodacom hawaingizi faida kuuuuubwa.
 
Ulitaka itolewe sh ngapi? Tuanze hapo
Hizi Ni sawa na US Dollars 100,000,000 ÷2,351 = 42,000 tu. Sasa ukae na kikosi cha thamani Kama Cha Simba na kocha wake kwa mwaka mzima, unadhani wewe walistahiki kulipwa ngapi?
 
Uwekezaji wa timu za Uingereza, na anachopata bingwa ni sawa?
Hii ni kote japo kwetu ni kidogo sana.
Timu zinatakiwa kubadilika, kuendeshwa kisasa ili zijiingizie faida.
Uingereza club inapata hela nyingi sana kutoka vyanzo tofauti vingi.
 
Mada kuu ni fedha anayopata bingwa.
Nafahamu kuwa Uingereza vyanzo ni vingi.
Ndo maana nikapendekeza vilabu viendeshwe kisasa.
Fafanua huo usasa unaosema, Nani hataki ligi ikiendeshwa kisasa? Kikwazo Ni Nini?
 
Ligi kuu ya Uingereza licha ya timu kuwekeza kwa gharama kubwa mshindi anapata £38M +haki za matangazo na makorokocho mengine jumla prize haizidi £155M.

Ilihali kuna timu zinatumia karibia £200M kwa ajili ya usajili tu. Wanapotuzidi wenzetu, wana sponsors wengi (klabu), mauzo ya jezi, mapato ya uwanjani.

Sasa huku timu inakadiriwa kua na mashabiki 5M+ inalipwa TZS 250M kwa msimu kama fedha ya mauzo ya jezi, kuna timu nyingine inapewa buku 3 kila mauzo ya jezi 1, hapa ndiyo utaona viongozi hamnazo kabisa. Jiulize kwanini zinashindwa kujenga uwanja walau wa mashabiki 30,000?

Simba au Yanga wanabidi wachangishe mashabiki, wanachama na wapenzi wao, wakope benki wajenge viwanja. Sio kwamba hii akili hawana, wanayo ila wapo kipigaji, hao kina Mo na GSM wapo kibiashara zaidi (faida kubwa wanapata wao) pumbafu sana...yaani UHL ni wakuishinda UMBRO kwenye tenda ya utengenezaji jezi za Simba?
 
Fafanua huo usasa unaosema, Nani hataki ligi ikiendeshwa kisasa? Kikwazo Ni Nini?
Nikisema klabu ziendeshwe kisasa namaanisha.
Kuwa na mfumo mzuri wa Uongozi utakao buni njia mbalimbali za mapato kama klabu.
Ikiwa ni pamoja na mauzo ya jezi, sponsors,....
 
Nikisema klabu ziendeshwe kisasa namaanisha.
Kuwa na mfumo mzuri wa Uongozi utakao buni njia mbalimbali za mapato kama klabu.
Ikiwa ni pamoja na mauzo ya jezi, sponsors,....
Bei halisi ya jezi original watanzania wengi hawawezi kuinunua kwasababu ya low purchasing power yetu, yaani ugali unakosekana sembuse kununua jezi?
 
Back
Top Bottom