Ligi kuu ya Uingereza licha ya timu kuwekeza kwa gharama kubwa mshindi anapata £38M +haki za matangazo na makorokocho mengine jumla prize haizidi £155M.
Ilihali kuna timu zinatumia karibia £200M kwa ajili ya usajili tu. Wanapotuzidi wenzetu, wana sponsors wengi (klabu), mauzo ya jezi, mapato ya uwanjani.
Sasa huku timu inakadiriwa kua na mashabiki 5M+ inalipwa TZS 250M kwa msimu kama fedha ya mauzo ya jezi, kuna timu nyingine inapewa buku 3 kila mauzo ya jezi 1, hapa ndiyo utaona viongozi hamnazo kabisa. Jiulize kwanini zinashindwa kujenga uwanja walau wa mashabiki 30,000?
Simba au Yanga wanabidi wachangishe mashabiki, wanachama na wapenzi wao, wakope benki wajenge viwanja. Sio kwamba hii akili hawana, wanayo ila wapo kipigaji, hao kina Mo na GSM wapo kibiashara zaidi (faida kubwa wanapata wao) pumbafu sana...yaani UHL ni wakuishinda UMBRO kwenye tenda ya utengenezaji jezi za Simba?