Tsh. 5000/= ya joining instruction form kibasila sekondari.

LIGEDENGE 1

Senior Member
Joined
Nov 15, 2013
Posts
184
Reaction score
29
Habari za jumapili wana jf. Mwenzenu nina mdogo wangu kachaguliwa kujiunga kidato cha 1 kibasila sec. Ya dsm . Cha ajabu naenda kuchukua fomu ya kujiunga,naambiwa nitoe tshs.5000, na wameweka tangazo kuhusu hilo. Toka lini shule za serikali wakadai pesa za joining.? Naomba ushauri ndugu zangu.
 
Wewe chukua join hiyo hela ni kwaajili ya kuandaa hyo form unayopewa kwanza mbona bei chee tu mjomba,
 
Wewe chukua join hiyo hela ni kwaajili ya kuandaa hyo form unayopewa kwanza mbona bei chee tu mjomba,

utata unakuja hapa,shuleni kwetu tunatoa fomu bure,na ni ya serikali. inakuwaje hapo? kwanini shule za serikali zitofautiane ktk utoaji fomu?
 
utata unakuja hapa,shuleni kwetu tunatoa fomu bure,na ni ya serikali. inakuwaje hapo? kwanini shule za serikali zitofautiane ktk utoaji fomu?

You have a point, ushauri wangu ni kuwa chukua hiyo form then udai payment receipt (halali not otherwise) maana malipo yoyote halali lazima yafanyike kwa receipt ili kesho au keshokutwa kama kutatokea maelekezo mbadala katika utoaji wa hizo form uweze kurudishiwa pesa yako. Watanzania msichukulie vitu kirahisi rahisi tu eti kwa sababu ni cheap hivyo uchukue tu bila kuhoji. Binafsi nakupongeza @LIGEDENGE, kwa kuhoji juu ya hili.
 
Waombe hiyo form ukatoe copy kwa sh.100 then uwarudishie original copy. Waache ujambazi
 

ahsante keen,maana siku hizi wizi wa kimaandishi ni mwingi
 
Jamani shule nyingine za serikali hali ipoje huko? Kuna urasimu kama huu?
 
utata unakuja hapa,shuleni kwetu tunatoa fomu bure,na ni ya serikali. inakuwaje hapo? kwanini shule za serikali zitofautiane ktk utoaji fomu?
Ruzuku zinafanana kwanini,je vyazo vya mapato vinalingana?ndomana sehemu zingine mchango wa taaluma 5000 na kwingine 30000,na kwingine hawachangii
 
ahsante keen,maana siku hizi wizi wa kimaandishi ni mwingi

Kila la kheri kwake mdogo wako, mwambie asome aache usharobaro, mjini shule, anaona kila kitu kulipia siku hizi, wameshindwa tu kutulipiza pumzi ya uhai! Hata hivyo, I believe kama hayo malipo ni halali lazima yawe kwa shule zote na standardized, otherwise ni UBUNIFU wa shule husika!
 
Sijawah kuona toka nianze kusoma! Ni juzi tu hapa Shy nilimfuatia dogo joining yake,ni bure kabisa tena hadi sample ya kitambaa wanabandika kwenye hyo karatasi na wanakuomba uwaambie na wengine wawahi kuchukua hizo form! TANZANIA BILA WIZI,HAIWEZEKANI
 
Ruzuku zinafanana kwanini,je vyazo vya mapato vinalingana?ndomana sehemu zingine mchango wa taaluma 5000 na kwingine 30000,na kwingine hawachangii

ndio maana kuna vijisenti vya taaluma,ulinzi,tahadhari n.k. hizo haziwatoshi hadi waje na kwenye fomu. wizi umezidi
 

pamoja keen. ila dogo tumempeleka private iringa. kibasila day hatomudu kwa jiji hili na kero zake ktk usafiri.
 

DAH MJINI WEZI WENGI. NDIO NASKIA SASA HIVI UTAPELI HUU. WAZAZI TUNAUMIZWA SANA. HUJAKAA SAWA TANESCO BEI JUU,GEUKA HUKU GESI JUU,MARA MAJI. wanataka turudi porini?
 
ulaji wa HeadMaster.
 

mkuu, mashule yetu yana matatizo sana. hii ni namna ya wewe kuchangia maendeleo ya shule. labda nashauri tu utoe huo mchango na baadae utakapoitwa kwenye kikao cha wazazi uhoji matumizi. hata ukienda kwenye vikao vya harusi kuna uchakavu. mbona masuala ya elimu inakuwa ishu?
 
wazo zuri,kibaya ni kuwa hupewi fomu hadi utoe 5 elfu yao

fomu haina kurasa moja tu. msilalamike sana kwani inawezekana makubaliano yalishafanywa na bodi ya shule kwa ajili ya suala fulani hapo shuleni. wazazi jengeni tabia ya kuhudhuria vikao mashuleni na muhoji mapato na matumizi
 
Nawewe acha kulia lia bwana,serikali yenyewe haikupeleki pesa za ruzuku,unadhani fomu wataandalia nini? Mbona taasisi nyingi za serukali kama vyuo vikuu fomu zinalipiwa tena pesa kibao hamhoji? hizo ni za maandalizi ya fomu,acheni mamabo ya bure bure kila wakati nyie.Halafu ulivyo mvivu wa kufikiri hata kuwauliza hapo hapo wakupe ufafanuzi hukutaka.Lipia fomu hiyo.











 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…