mkuu, mashule yetu yana matatizo sana. Hii ni namna ya wewe kuchangia maendeleo ya shule. Labda nashauri tu utoe huo mchango na baadae utakapoitwa kwenye kikao cha wazazi uhoji matumizi. Hata ukienda kwenye vikao vya harusi kuna uchakavu. Mbona masuala ya elimu inakuwa ishu?
fomu haina kurasa moja tu. Msilalamike sana kwani inawezekana makubaliano yalishafanywa na bodi ya shule kwa ajili ya suala fulani hapo shuleni. Wazazi jengeni tabia ya kuhudhuria vikao mashuleni na muhoji mapato na matumizi
shule za private kuna ada tena kubwa tu. Lakini hata fomu za kujiunga zinalipiwa. Tena ipo michango kama ya masomo ya remedial, computers n.k.nje ya ada. Hii ndo maana masomo yanaimarika kwa sababu yako fully financed.
Kati shule za serikali fedha ni kiduchu sawa na dose moja ya malaria kugawia wagonjwa kumi. Malaria itapona kweli. Kama jibu ni hapana basi hata elimu kwenye shule zetu haitaimarika ikiwa wote tunalalamika hata kwa elfu tano ya fomu!
nawewe acha kulia lia bwana,serikali yenyewe haikupeleki pesa za ruzuku,unadhani fomu wataandalia nini? Mbona taasisi nyingi za serukali kama vyuo vikuu fomu zinalipiwa tena pesa kibao hamhoji? Hizo ni za maandalizi ya fomu,acheni mamabo ya bure bure kila wakati nyie.halafu ulivyo mvivu wa kufikiri hata kuwauliza hapo hapo wakupe ufafanuzi hukutaka.lipia fomu hiyo.
ulaji wa headmaster.
kama zingetumika kwa maendeleo ya shule sina tatizo. Kinachouma pale shule hakuna mabadiliko,zaidi mabadiliko yapo kwenye miili ya watu
sawa hata umeme. maji na vtu vingine ni tatizo. sasa mkae mjadili namna ya kuondoa tatizo la kukaa chinihuko private sawa,ila huku serikalini vimichango vingiii...lakn wanetu bado wanakaa chini wakati wa masomo