Tsh Milion tatu (3,000,000) tasilimu


daaa hii tamu sana mkuu hapo niomekupata and thank you much nitakupa mrejesho
 
Fanya hivi:

  1. Nunua ardhi ekari moja - Tshs 500,000/- max. Ardhi hii iwe inafaa kwa ajili ya kufuga nyuki. Kwa Morogoro jaribu maeneo ya Mikese, vijii nyuma ya Sangasanga (mf: Mafuru), Mkundi kwa mbele n.k.
  2. Nunua mizinga 10 ya kisasa ya nyuki (commercial beehives) - Tshs 1,200,000/-.
  3. Installation cost ya mizinga + usafiri - Tshs 350,000/-

Baada ya miezi sita - ceteris paribus:
  1. Kila mzinga utatoa lita 30 - 40.
  2. Utauza asali kwa Tshs 10,000/-
  3. Jumla ya mapato kwa mvuno mmoja itakua Tshs 3,000,000 - 4,000,000/-
  4. Utavuna mara mbili kwa mwaka i.e pato hapo juu *2

Kila la kheri!
 
Reactions: bdo
Wenzio sembe wanamaanisha cocaine,wewe vipi!

nilimemuelewa sana ila dawa ya uhuni ni jeuri.mm nimekuja kuomba ushauri sasa yy anafanya uhun ndo maana namletea jeuri ya kuwa ktk dunia ya nne.thanks
 

much appreciation for the nice idea
 
Reactions: bdo

Kaka wazo zuri zaidi...na wengine tumepata jifunza fursa hiyo na kuongeza ktk mawazo yetu. Ila je vipi kuhusu soko lake kwa sasa maana watu wengi wameanza kutoamini asali kwa kubambikiwa na wateja wanapungua!! Pia challenge nyingine ni upatikanaji wa mizinga. Una details za eneo kwa moro ambalo wanatoa huduma hii. Asante kaka mkuu.
 
Ila je vipi kuhusu soko lake kwa sasa maana watu wengi wameanza kutoamini asali kwa kubambikiwa na wateja wanapungua!! Pia challenge nyingine ni upatikanaji wa mizinga. Una details za eneo kwa moro ambalo wanatoa huduma hii. Asante kaka mkuu.

Mkuu 0909Hekima,

Uchakachuaji wa asali ni changamoto inayokua kwa kasi sana nchini mwetu, hili linachangiwa sana na wafanyabiashara na wafuga nyuki wasio waaminifu. Uhitaji wa asali bado ni mkubwa na unaendelea kukua kwa kasi ndani na nje ya Tanzania, cha kuzingatia ni kuwa na asali bora inayokidhi viwango vinavyohitajika. Mfano hai wa hili ni kiwanda cha kusindika asali kilichopo Visiga Kibaha kushindwa kufikia lengo lake la ununuzi asali toka wafuga nyuki mwaka jana kutokana na ubora duni wa asali.

Elimu ya ufugaji bora wa nyuki na uvunaji mzuri wa asali na mazao mengine ya nyuki utasaidia kupunguza tatizo la ubora duni. Kwa Morogoro, maeneo mengi wanauza mizinga, mfano SUA (Idara ya Misitu), Kihonda Viwandani n.k. Pia kuna watengenezaji wengi mitaani wa mizinga. Cha kuzingatia ni aina na ubora wa mizinga ya kutumia.

Karibu kwenye ufugaji nyuki! Kwa maelezo yoyote na msaada kuhusu ufugaji nyuki tafadhali tuwasiliane.
 
Allan
Kwani ni vigezo gani ardhi inatakiwa kuwa navyo ili kufuga nyuki
 

Asante kaka mkuu, hapo nimekuelewa na mi pia nimeshawishika na jambo hili. Nitakupa feedback.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
kaka kuna kampuni moja inaitwa jibu huko Arusha ukiweka hiyo kwa mwezi unachukua kama 250000/=riba ambayo inakua ten percent baada ya makato ya TRA kwa hiyo ndani ya mwaka hivi utakua uko poa kabisa wewe ukiwa unafanya michakato mingine.
 

mkuu nimekupata vp soko lake maana nina aslio imechujwa kitaalamu kwa usimamizi wa watu wa maliasili ninayo ya kutosha sana mm huwa ninanunua kigoma kama unamfahamu mtu anayenunua niunganishe nae nina mzigo wa kutosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…