Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,506
Mkuu 0909Hekima,
Uchakachuaji wa asali ni changamoto inayokua kwa kasi sana nchini mwetu, hili linachangiwa sana na wafanyabiashara na wafuga nyuki wasio waaminifu. Uhitaji wa asali bado ni mkubwa na unaendelea kukua kwa kasi ndani na nje ya Tanzania, cha kuzingatia ni kuwa na asali bora inayokidhi viwango vinavyohitajika. Mfano hai wa hili ni kiwanda cha kusindika asali kilichopo Visiga Kibaha kushindwa kufikia lengo lake la ununuzi asali toka wafuga nyuki mwaka jana kutokana na ubora duni wa asali.
Elimu ya ufugaji bora wa nyuki na uvunaji mzuri wa asali na mazao mengine ya nyuki utasaidia kupunguza tatizo la ubora duni. Kwa Morogoro, maeneo mengi wanauza mizinga, mfano SUA (Idara ya Misitu), Kihonda Viwandani n.k. Pia kuna watengenezaji wengi mitaani wa mizinga. Cha kuzingatia ni aina na ubora wa mizinga ya kutumia.
Karibu kwenye ufugaji nyuki! Kwa maelezo yoyote na msaada kuhusu ufugaji nyuki tafadhali tuwasiliane.
Safi sana mkuu, haya ndiyo mambo tunatakiwa tuyapate hapa JForums.
Kwa suala la asali kama nikiivuna tayari na nikaamua kuisafirisha kuja Dar es Salaam, ninaweza kukaa nayo siku ngapi bila kuharibika??
Au mpaka niichemshe??