Tsh Milion tatu (3,000,000) tasilimu


Safi sana mkuu, haya ndiyo mambo tunatakiwa tuyapate hapa JForums.

Kwa suala la asali kama nikiivuna tayari na nikaamua kuisafirisha kuja Dar es Salaam, ninaweza kukaa nayo siku ngapi bila kuharibika??

Au mpaka niichemshe??
 
mkuu asigwa bei ya mizinga inafikia kiasi gani kwa sasa!kama hapa moro ninashamba mikese.thanks
 
Nasahukuru wa kuu kwa michango yenu kwa sasa niliamua kuanza na asali lakin kabla sijaanza kufuga nyuki nimeamua kuanza kununua ili nijue market nina mzigo tayari pia mnakaribishwa kuniunga mkono.nataraji baada ya miez mitatu ninunue shamba nifuge mbuzi kadhaa kwani niko ktk mchakato wa kupata ardhi na nimeongea na manispa na wanaanza kugawa soon
 

Mkuu haya mawazo yako yamenikuna sana, Naomba kuuliza maswali ya msingi mawili matatu....

Hekari moja inaweza kuchukua mizinga mingapi kitaalamu na kibongo bongo inakaa mingapi??

Kama nitapata eneo la hekari say 50 nikaanzisha bustani yangu mwenyewe ya maua, je production inaweza kupanda kwa kuwa malighafi ya kutengeneza asali inakua karibu na nyuki hawawezi kwenda mbali??

Kwa uelewa wako binafsi vipi soko la asali kwa mtu anayezalisha mzigo mkubwa kwa mwaka??

Thanks in advance
 
mkuu asigwa bei ya mizinga inafikia kiasi gani kwa sasa!kama hapa moro ninashamba mikese.thanks

Mkuu kama unataka kuendesha kibiashara zaidi bei ya mzinga wa kutosha kutoa lita 40 kwa mara moja ie lita 80 kwa mwaka ni tsh 120,000 kama utataka kununua ile ya kitaalamu ila kbongo bongo inakwenda mpaka 60 au 70 hivi.
 
Mkuu bdo hebu weka humu elimu ya ufugaji wa mbuzi, inaonekana umekomaa katika sehemu hii. Unajua mbuzi kama kilimo ni njia muafaka ya kuachana na huu "umasikini" tunaoelezewa. Funguka mkuu bdo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…