Tshabalala na Kapombe imetosha sasa

Edson Carrington

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2022
Posts
216
Reaction score
636
Habari wakuu,

Nadhani imefikia pahala Simba haina budi kutafuta suluhisho za beki hizi kongwe zitokazo pembeni.

Hii kutokana na kuchoka kimwili mpaka kiakili haswa linapokuja suala la maamuzi ya haraka na ukabaji kwa ufasaha kama walivyokuwa awali.

Tshabalala anashindwa win wipira mingi sana akikaba, na pia amekuwa mwepesi wa kupoteza mipira jambo ambalo linacost team kwa kiasi kikubwa sana.

Kapombe kwa sasa hana uwezo wa kufanya marking kabisa. Amekuwa uchochoro kwa washambuliaji na pia pale anapokuwa na mipira haswa huwaza zaidi kutoa krosi zaidi ya hapo hana mbinu nyingine mbadala. Pia amekuwa mzito kupandisha mashambulizi kwenye upinzani.

Me naona ni muda muafaka sasa kuwapumzisha maveterani hawa kwa upande wetu, kwani tayari wamekwisha choka na wanashindwa kuendana na kasi ya club katika kutafuta matokeo.

Zaidi ya hayo, tunawaheshimu na tunathamini mchango wao.
 
Kapombe sifuri yule
 
Bora muwe mnaulizia tunawasaidia mtakufa na UPUMBAVU WENU.

1. Level ya Wachezaji wa Alhaly IPO juu sana kulinganisha na Simba.
Uimara WA Alhaly ni Maeneo ya Pembeni, ndio wako Bora zaidi.

2. Eneo analocheza beki wa kulia mtu wa kwanza kutoa msaada Huwa anakuwa No 7 ambaye mara Nyingi anakuwa KIBU. Jana KIBU alichezeahwa No 9 na
(Jana no 7 Alikuwa Miquisson aliyeisha na kuchoka vibaya kabisa.

3. Msaada Mwingine WA Kumsaidia No 2 ni Beki No 5 ambaye ni Inonga ambaye Majeraha Yameshusha sana Uwezo wake.
Amepata Majeraha mara tatu ndani ya KIPINDI Cha Muda Mfupi


4. Yote ya yote Simba wanaathirika sana kutokana na kukosa kiungo WA Asili kabisa WA UKABAJI.
Hili nimelisema zaidi ya mala 1000 sasa.

Karibu kwa swali lingine

MUWE MNAJIFUNZA MPIRA AU MNATAG KUULIZA
 
Same same to Shabalala...

Winga wa shabalala ni chama ndio 11 WA Simba unategemea atakaba...

Msaada wa karibu WA pili ni Mzamiru ambaye Jana Alikuwa mbovu kupita maelezo.

Chemalone na shabalala Wana Uelewano mzuri mno tofauti na Onyango WA kuchomeaha.

( Ya wakulamiwa ni mo Kusajili akina Ayoub.

SIMBA KATIKA WACHEZAJI 9 WALIOSAJILI NI WAWILI TU WENYE UWEZO.
 
Shabalala akipewa mpira anaanza kufikiri kwanza, Kuna kipindi badala ya kutoa pasi kwa Saidoo anapiga Kross ambayo haina macho.
 
Simba nyie ni wasengerema sana,timu ikipanda haishuki inawaachia mabeki ,Sasa timu ya hivi ijiandae kubugia mengi ikizingatiwa Winga za Al Ahly ziko vizuri na timu Yao inapanda yote na inashuka yote.
 
Simba nyie ni wasengerema sana,timu ikipanda haishuki inawaachia mabeki ,Sasa timu ya hivi ijiandae kubugia mengi ikizingatiwa Winga za Al Ahly ziko vizuri na timu Yao inapanda yote na inashuka yote.
Kijana kwani mechi ya jana si imetoka mbili mbili ama?
Kwagyo sisi hatushuki haraka lakini tunaweza kuwafunga goli mbili watu wanashuka haraka basi sio mbaya
 
Kijana kwani mechi ya jana si imetoka mbili mbili ama?
Kwagyo sisi hatushuki haraka lakini tunaweza kuwafunga goli mbili watu wanashuka haraka basi sio mbaya
Mumeponea bahati mlikuwa mnakula 4 ,Kwa hiyo usijifariji sana
 
Ungeweza tu kutoa maoni yako na ungeeleweka vizuri bila ya kejeli
 
Ila tujiulize hao wachezaji wanapangwa kwa maelezo ya viongozi au kocha tukishajua ndio tuelekeze lawama kwake
 
Ndo maana kocha wa Taifa Stars akaona isiwe tabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…