Tshabalala na Kapombe imetosha sasa

Tshabalala na Kapombe imetosha sasa

Habari wakuu,

Nadhani imefikia pahala Simba haina budi kutafuta suluhisho za beki hizi kongwe zitokazo pembeni.

Hii kutokana na kuchoka kimwili mpaka kiakili haswa linapokuja suala la maamuzi ya haraka na ukabaji kwa ufasaha kama walivyokuwa awali.

Tshabalala anashindwa win wipira mingi sana akikaba, na pia amekuwa mwepesi wa kupoteza mipira jambo ambalo linacost team kwa kiasi kikubwa sana.

Kapombe kwa sasa hana uwezo wa kufanya marking kabisa. Amekuwa uchochoro kwa washambuliaji na pia pale anapokuwa na mipira haswa huwaza zaidi kutoa krosi zaidi ya hapo hana mbinu nyingine mbadala. Pia amekuwa mzito kupandisha mashambulizi kwenye upinzani.

Me naona ni muda muafaka sasa kuwapumzisha maveterani hawa kwa upande wetu, kwani tayari wamekwisha choka na wanashindwa kuendana na kasi ya club katika kutafuta matokeo.

Zaidi ya hayo, tunawaheshimu na tunathamini mchango wao.
beki gani mwingine anaweza kuwabadili? ila tungekuwa na beki imara jana, waarabu walikuwa wanafungwa. tulishawakamata wakarudi wote kulinda goli na walifurahi kweli mpira kuisha. hatuna mabeki wenye mbio kukabili counter attack. siku zote waarabu huwa wanatufunga kwa counter attack ila kwa hii kawaida tunawamudu. unaweza kushangaa tumewakamataaa muda mrefu,wanakuja kupiga counter attack moja au mbili wanakuwa mbele. kwanini hatujiandai kwa counter attack?
 
Bora muwe mnaulizia tunawasaidia mtakufa na UPUMBAVU WENU.

1. Level ya Wachezaji wa Alhaly IPO juu sana kulinganisha na Simba.
Uimara WA Alhaly ni Maeneo ya Pembeni, ndio wako Bora zaidi.

2. Eneo analocheza beki wa kulia mtu wa kwanza kutoa msaada Huwa anakuwa No 7 ambaye mara Nyingi anakuwa KIBU. Jana KIBU alichezeahwa No 9 na
(Jana no 7 Alikuwa Miquisson aliyeisha na kuchoka vibaya kabisa.

3. Msaada Mwingine WA Kumsaidia No 2 ni Beki No 5 ambaye ni Inonga ambaye Majeraha Yameshusha sana Uwezo wake.
Amepata Majeraha mara tatu ndani ya KIPINDI Cha Muda Mfupi


4. Yote ya yote Simba wanaathirika sana kutokana na kukosa kiungo WA Asili kabisa WA UKABAJI.
Hili nimelisema zaidi ya mala 1000 sasa.

Karibu kwa swali lingine

MUWE MNAJIFUNZA MPIRA AU MNATAG KUULIZA
Ulivyoongelea Upumbavu tu, sijaendelea kusoma.
Jifunze nidhamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba nyie ni wasengerema sana,timu ikipanda haishuki inawaachia mabeki ,Sasa timu ya hivi ijiandae kubugia mengi ikizingatiwa Winga za Al Ahly ziko vizuri na timu Yao inapanda yote na inashuka yote.
Sasa kukaba na wote na kushambulia wote ni strategy ambayo Simba haitumii,
Huwezi badilisha mfumo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hata chama jana kazingua sana, anapiga pasi kama anacheza na mtibwa, waarabu wakawa wanajiokotea tu. mwambieni awe serious na yeye anaenda akizeeka.
 
beki gani mwingine anaweza kuwabadili? ila tungekuwa na beki imara jana, waarabu walikuwa wanafungwa. tulishawakamata wakarudi wote kulinda goli na walifurahi kweli mpira kuisha. hatuna mabeki wenye mbio kukabili counter attack. siku zote waarabu huwa wanatufunga kwa counter attack ila kwa hii kawaida tunawamudu. unaweza kushangaa tumewakamataaa muda mrefu,wanakuja kupiga counter attack moja au mbili wanakuwa mbele. kwanini hatujiandai kwa counter attack?
Ndio maana nikasema kuwabadilu wakongwe hawa ni process maalum inaweza kutumika,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mfumo wanaocheza Simba Mohamed Hussein na Kapombe wanafanya kazi mbili kwa wakati mmoja. Timu inaposhambulia wanakuwa mawinga na timu inaposhambuliwa wanarudi kuwa mabeki. Tatizo linaanzia pale ambapo timu inashambulia halafu mpira umechukuliwa na adui. Hapo ndipo unategemea kuona kiungo mkabaji akichukua nafasi zao wakati wao Kapombe na Tshabalala wanatakiwa warudi haraka kwenye nafasi zao.

Lakini kwa sasa ilivyo Simba kuna tatizo la kiungo mkabaji mwenye kasi na uwezo wa kunusa hatari pindi inapotokea mabeki wa pembeni wameenda kushambulia. Lakini kuna shida nyingine ambayo ni namna Kapombe na Mohamed Hussein wanavyotumika kwenye mechi nyingi mfululizohata za kirafiki kwa zaidi ya miaka mitatu sasa. Ni wakati sasa wa kuanza kuwapa mapumziko kwenye baadhi ya mechi Simba inapokutana na timu ndogo ndogo au mechi za kirafiki. Vile vile benchi la ufundi liwe linawapumzisha pale Simba inapokuwa inaongoza kwa goli nyingi dhihi ya wapinzani wao.

Nikiitazama ligi yetu kwa sasa bado nawaona Kapombe na Mohamed Husein bado wana nafasi ya kucheza Simba kwani hata waliopo kwenye timu za ligi wanauwezo tu sawa na wao na hata kama kuna waliowazidi basi ni mmoja au wawili na wapo kwenye timu hizi kubwa tatu. Kikubwa benchi la ufundi liwapunguzie majukumu ili miili yao nayo ipumzike kwani wao ni bindamu na sio mashine.
 
Ungeweza tu kutoa maoni yako na ungeeleweka vizuri bila ya kejeli
Mkuu kuna watu bila kuwakejeli kidogo hawajifunzi kwakua hawaujui mpira hua wanamihemko tu.

Full back ya kulia anasaidiwa na watu watatu namba 7,8 na namba 5 na full back ya kushoto anasaidiwa na namba 11,6 na namba 4 hizi combination zikielewena vizuri hua ni msaada sana kwenye timu

Strength kubwa ya Kapombe iko kwenye attacking Kapombe anapenda sana kushambulia ana hayo matamanio, sasa mwalimu ni lazima ajue hilo na kuwapa watu wengine majukumu ya kumkabia anapokua hayupo.

Kama Robertinho angakua na mifumo mingi angeweza kutumia mfumo wa back three hii ingemfaa sana Kapombe kucheza kama right wing back hua ana hatari sana akicheza hii position

Kuna kipindi wakati Kapombe yuko Azam kuna mwalimu alikua anatumia huu mfumo ulimfaa sana kapombe alimalizaga ligi akiwa na magoli na assists za kutosha..

Kapombe bado ni mchezaji mzuri tu hizi sifa ata Mohamedi hussein anazo pia, mohammed hussein yeye hutumia akili zaidi kukaba kuliko nguvu kwakua hana nguvu za kutosha kuweza kukabiliana na washambuliaji wenye mabavu, hivyo huitaji sana back up ya haraka ambayo ikikosekana huonekana uchochoro.

Pamoja na hayo bado ni left full back bora kabisa.
 
Bora muwe mnaulizia tunawasaidia mtakufa na UPUMBAVU WENU.

1. Level ya Wachezaji wa Alhaly IPO juu sana kulinganisha na Simba.
Uimara WA Alhaly ni Maeneo ya Pembeni, ndio wako Bora zaidi.

2. Eneo analocheza beki wa kulia mtu wa kwanza kutoa msaada Huwa anakuwa No 7 ambaye mara Nyingi anakuwa KIBU. Jana KIBU alichezeahwa No 9 na
(Jana no 7 Alikuwa Miquisson aliyeisha na kuchoka vibaya kabisa.

3. Msaada Mwingine WA Kumsaidia No 2 ni Beki No 5 ambaye ni Inonga ambaye Majeraha Yameshusha sana Uwezo wake.
Amepata Majeraha mara tatu ndani ya KIPINDI Cha Muda Mfupi


4. Yote ya yote Simba wanaathirika sana kutokana na kukosa kiungo WA Asili kabisa WA UKABAJI.
Hili nimelisema zaidi ya mala 1000 sasa.

Karibu kwa swali lingine

MUWE MNAJIFUNZA MPIRA AU MNATAG KUULIZA

Bahati Jana Al Ahly walikua wanacheza kwa kurelax sana maana wanajua mechi wanaimaliza Cairo! Ila jana hasa kipindi cha kwanza tulikua tunakula goli 4!
Timu nzima inapanda kushambulia kama mang’ombe nyuma inaacha nafasi kubwa ila wakati wa kurudi kuzuia watu “wanajog” bila wasiwasi!
Malengo ya nusu fainali CAFCL ni makubwa sana kwa timu hii.
 
Lakini Perci Tau akaomba kutoka
Tau angekuwa amatulia angeweza kuondoka na goal 2 za wazi kabisa ila Kapombe nilimuonea huruma jana maana zile winger 2 yule Slim ni balaa akaja kuingia nuksi zaidi Shehati yaani walikuwa wanajifanyia wanavyotaka tu. Mimi nadhani formation Simba hawakuwa na watu wa kutoa msaada kwa Kapombe na Mohd, Nadhani mchezo wa Cairo kupunguza yale makali ya winger zao ni kucheza 352 kwa maana hii kuna watu kama Chama na Said kutokupangwa sio kwa sababu wabaya hapana mfumo, lakini kama tutaenda na same formation 433 inabidi 451 ili Kibu kulia na kushoto sijui nani acheze ili wa track back kusaidia fullbacks. Al Ahly hatari wakitokea pembeni wana speed na technical wako vizuri ila tukienda na Chama na Saido basi Simba watafungwa tu hakuna namna.
 
Tumetoa draw na mabingwa wa Africa halafu anakuja mtu anataka tusikitike......

Al ahly hata wengetufunga hakuna mtu mwenye akili timamu angeshangaa...
 
Back
Top Bottom