Tsn yapata mwenyekiti na bodi mpya

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2008
Posts
2,268
Reaction score
335
BREKING NYUUUUUUZZZZZ:TSN YAPATA MWENYEKITI NA BODI MPYA

Bw. Wilson Mukama


RAIS JAKAYA KIKWETE AMEMTEUA BW WILSON MUKAMA KUWA MWENYEKITI MPYA WA BODI YA WAKURUGENZI YA MAGAZETI YA SERIKALI (DAILY NEWS NA HABARI LEO CHINI YA TANZANIA STANDARD NEWSPAPERS LTD - TSN) KUANZIA FEBRUARY 26, 2010.

BW. MUKAMA ALIWAHI KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII NA AMESTAAFU HIVI KARIBUNI AKIWA KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI. ALIWAHI PIA KUWA MKURUGENZI WA JIJI LA DAR.

KWA MUJIBU WA TAARIFA ILIYOTOLEWA JIONI HII, KUFUATIA UTEUZI HUO WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO MH. GEORGE MKUCHIKA AMEWATEUWA WAJUMBE WANNE KUUNDA BODI YA TSN KAMA IFUATAVYO:

1. BI. HIJA HAWA MANGA AMBAYE NI MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA PENSHENI WA WATUMISHI WA UMMA (PSPF)

2. BW. KALUA SIMBA (MCHUMI WA KUJITEGEMEA KUTOKA SEKTA BINAFSI

3. BW. CLEMENT MSHANA (MKURUGENZI IDARA YA HABARI - MAELEZO)

4. BW. CHARLES RAJABU (AFISA HABARI MKUU DARAJA LA KWANZA, WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO.



Source: Michuzi blog
 
BW. MUKAMA ALIWAHI KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII NA AMESTAAFU HIVI KARIBUNI AKIWA KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI. ALIWAHI PIA KUWA MKURUGENZI WA JIJI LA DAR.

Hii inaonyesha hakuna vijana wa kufanya hizi kazi, au ndo ule msemo na sera ya CCM kuwa vijana ni Taifa la kesho? Je hiyo kesho itafika lini?
 
when is the recycling program gonna end?
Mkuu Mwanakijiji

Hili suala nimekuwa najiuliza kila siku;

yaani mtu akiwa anastaafu anajijengea mazingira ya kubaki katika serikali

1.Huyo mama Mamanga anastaafu ukurugenzi mwaka huu
2.Mukama same story

hivi kwanini wasikatae madaraka kwa kigezo cha kustaafu?

Between the line,hivi tunau gonjwa gani coz hata wabungwe wakiambiwa wawekee kikomo cha uongoziu hawataki..

watu wale wale,madudu yale yale na wanendelea kulindana..shamba la bibi bwana..
 
Kawaida ya mtu hugeuka kuwa tabia yake.

Kitu kingine kinachofanana na hiki ni mtu kuwa mbunge halafu anateuliwa kuwa mkuu wa mkoa, hivi vigezo ni vipi, ni kweli kuwa sisi vijana hatuonekani kabisa?
 
Du1 inasikitisha sana mtu kama huyu ameshashika nyadhifa kibao na alishastaafu lakini bado anarudishwa kazini, hivi kuna maana gani kutuambia amestaafu? hivi nchi hii hakuna vijana wanaoweza kufanya kazi? kwa nini hawa wazee wanajifanya wao ndiyo wakuu tuu? inauma sana, hata baba zetu tunakula nao majumbani kumbe hawapendi tupate kazi kama za kwao, sijui watusomesha ili tufanye nini, PUMBAVU sana.
 
Kawaida ya mtu hugeuka kuwa tabia yake.

Kitu kingine kinachofanana na hiki ni mtu kuwa mbunge halafu anateuliwa kuwa mkuu wa mkoa, hivi vigezo ni vipi, ni kweli kuwa sisi vijana hatuonekani kabisa?
Pale pale anatakiwa kusimamia maendeleo ya jimbo lake, pia anatakiwa aangalie maendeleo ya mkoa wake anaoongoza nikisema mkoa mpaka na wilaya zake. unajua nini kitakachofata!! muda mrefu atakuwa jimboni kwake akiuza sura kwa ajili ya uchaguzi ujao.Swali pindi kampeni zitakapo anza huyu mkuu wa mkoa atakwenda jimboni kwake kwa muda wote huo kupiga kampeni je ninani atakaeongoza huo mkoa?
 
]... hata baba zetu tunakula nao majumbani kumbe hawapendi tupate kazi kama za kwao, sijui watusomesha ili tufanye nini, PUMBAVU sana.[/B]
Mkuu punguza hasira, ona sasa unamtukana baba yako!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…