Ng'wanza Madaso
JF-Expert Member
- Oct 21, 2008
- 2,268
- 335
BREKING NYUUUUUUZZZZZ:TSN YAPATA MWENYEKITI NA BODI MPYA
Bw. Wilson Mukama
Source: Michuzi blog
Bw. Wilson Mukama
RAIS JAKAYA KIKWETE AMEMTEUA BW WILSON MUKAMA KUWA MWENYEKITI MPYA WA BODI YA WAKURUGENZI YA MAGAZETI YA SERIKALI (DAILY NEWS NA HABARI LEO CHINI YA TANZANIA STANDARD NEWSPAPERS LTD - TSN) KUANZIA FEBRUARY 26, 2010.
BW. MUKAMA ALIWAHI KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII NA AMESTAAFU HIVI KARIBUNI AKIWA KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI. ALIWAHI PIA KUWA MKURUGENZI WA JIJI LA DAR.
KWA MUJIBU WA TAARIFA ILIYOTOLEWA JIONI HII, KUFUATIA UTEUZI HUO WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO MH. GEORGE MKUCHIKA AMEWATEUWA WAJUMBE WANNE KUUNDA BODI YA TSN KAMA IFUATAVYO:
1. BI. HIJA HAWA MANGA AMBAYE NI MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA PENSHENI WA WATUMISHI WA UMMA (PSPF)
2. BW. KALUA SIMBA (MCHUMI WA KUJITEGEMEA KUTOKA SEKTA BINAFSI
3. BW. CLEMENT MSHANA (MKURUGENZI IDARA YA HABARI - MAELEZO)
4. BW. CHARLES RAJABU (AFISA HABARI MKUU DARAJA LA KWANZA, WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO.
Source: Michuzi blog