KERO TTCL Corporation, Kum-block mteja Facebook kwa kuuliza swali si sawa

KERO TTCL Corporation, Kum-block mteja Facebook kwa kuuliza swali si sawa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwanza kabisa TTCL ni shirika la umma, linaendeshwa kwa kodi zetu sisi wananchi.

Pili, admin wote wa social networks ikiwa ni pamoja na Facebook wanalipwa mshahara kutokana na kodi zetu sisi wananchi, ni watumishi wetu wananchi.

Tatu mnatumia social networks zenu kutoa taarifa kwa umma kuhusu shirika lao na huduma mnaziwapatia ambazo wanazilipia, hawaombi wala hawakopi, ni kodi zao zipo kazini.

TTCL sio mali ya mtu binafsi, haiendeshwi kwa fedha kutoka mfukoni kwa mtu, same applies kwa social networks zote za TTCL.

Kifaa mnachotumia kupost huduma za shirika, umeme mnaotumia, internet mnayotumia na mshahara wenu vyote ni kodi zetu wananchi.

Inasikitisha mwananchi ninapouliza swali kuhusu huduma fulani, kwa kutumia lugha ya staha kabisa, ili nipate uelewa kuhusu huduma ya shirika langu la umma halafu admin ananiblock, bila onyo bila maelezo.

FB_IMG_1774176007455.jpg


Mnakiuka haki zangu kama mwananchi na mteja wa shirika la umma ambalo mmepewa dhamana ya kuliendesha kwa muda, kufanya maamuzi kwa mihemko yenu binafsi.

Mnategemea nitapataje taarifa kuhusu huduma za shirika langu? Kwa sababu jioni niliuliza kitu kuhusu huduma yenu mliyozindua karibuni ya supersonic expirience, ghafla asubuhi naamka nipo blocked out of the blue. Ingekua ni shirika binafsi au account binafsi ningeelewa.

Wananchi huku mtaani na hata kwenye comment za social networks zenu zote wanaonesha kutokua na imani na hili shirika la TTCL sana, sasa nyie ma admin mnaongeza chumvi kwenye kidonda kwa kuwanyima wanachi haki ya ku interact na shirika lao, kuona huduma, kutoa taarifa na kupokea mrejesho.

Watu tunajitahidi kutoka mitandao mingine na kuanza kutumia huduma zenu nyie mnatuzuia, halafu mnasema rudi nyumbani kumenoga. SHAME SHAME SHAME!
 
Unashangaa ya TTCL, Huko Twitter na Instagram Rais wa nchi anawablock wananchi wake kwa speed kama upepo.
 
Back
Top Bottom