TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Hivi kwa mfano nilinunua bando la internet la mwez .....kabla halijaisha nikanunua tena la siku. Je kwa mda huo ni lipi litatumika
 
Usije ukarogwa ukaingia mkenge.
Hizo GB 4 .usishangae ukawekewa limit mchana tumia GB 1 zingine utumie usiku
Nikiona watanzania mnavyo sifia makampuni ya mabepari wakakati kampuni ya kizawa TTCL ipo tu kwa muda mrefu na ufanisi hafifu, na watumishi wake wa kizawa ila hawaoni umhim wa kufanya maboresho chap chap ili kuteka soko, najisikia vibaya saana.

Ilitakiwa mtumbuliwe wote, waanze moja.

Yani makampuni mengine yana ringa hatari, vifurushi vina badilika kila saa.
Asubuhi unajiunga na hiki, ukikifuatilia tena hukikuti tena, kipo kingine.
Hadi nimewaza nikasema labda siku hizi kuna vifurushi ONE TIME BUNDLE,
yani ukijiunga mara moja unapoteza sifa za hilo bando. Hahahaha

POLE TANZANIA YETU.
 
Kwenye kuangalia salio la kifurushi chako kupitia *148*30# ni majanga. Kila ukiangalia unaambiwa "Ujumbe wa salio la kifurushi chako utatumwa punde" Lakini utasubiri sana na hautatumwa. Nina mwezi mzima kila nikiangalia salio la kifurushi cha SMS hawatumi ujumbe kwamba SMS ngapi ninazo na ngapi zimetumika. UTENDAJI MZIGO KABISA.
 
Siku ya tatu leo napambana kuhamisha kiasi cha pesa kutoka tigo pesa kwenda T-pesa bila mafanikio ila kwenda mitandao mingine huduma kama kawaida, nini tatizo?
 
Kwahiyo TTCL mmeona kutaja OFFICE za daresalaamu tu. Maana Dar ndo Tanzania nzima au mmekuja humu kutu enjoy . Wewe unahudumia darselam au Tanzania nzima!? .mnakera sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…