TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Huu mtandao sijawahi kuvutika kuutumia kabisa kwa sababu huku niliko sijawahi kuona hata wakala wa TTCL. Changamkeni aisee.
Pole kwa changamoto hiyo,tafadhali tufahamishe unapatikana maeneo gani ili tufuatilie na kutatua.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
 
Hawa majamaa ni wahuni sana hawa yaani nimejiunga GB 10 ili nipakue vitu vangu chaajabu network ipo slow kama kinyonga.

Kesho asubuhi alfajiri na mapema naivunjavunja laini yao kwa meno yangu.
Uzi tayari.
TTCL
Pole kwa changamoto hiyo,tafadhali tufahamishe unapatikana maeneo gani ili tufuatilie na kutatua.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
 
TTCL wao ndio wamiliki wa mkongo wa taifa wa fiber, nashindwa kuelewa kwanini wako slow?
Pole kwa changamoto hiyo,tafadhali tufahamishe unapatikana maeneo gani ili tufuatilie na kutatua.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
 
Data traffic ya ttcl kiukweli huwa inasumbua ukiwa mijini, mfano huku mitaa ya sinza inaenda 4-6mbps ila ukiwa maeneo kama tegeta huwa spidi ni 24-39mbps.
Hiyo ni kwa line za 4G
Pole kwa changamoto hiyo,tafadhali tufahamishe unapatikana maeneo gani ili tufuatilie na kutatua.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
 
Dah nilijua ni mm peke yangu imenikuta hii juzi tu hapo aseeh nilikasirika mnoo mpaka asubuhi hakuna nilichokamilisha kupakuwa
[emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35]
Pole kwa changamoto hiyo,tafadhali tufahamishe unapatikana maeneo gani ili tufuatilie na kutatua.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
 
Hicho kifurushi kitakuwa mahususi kwa dakika, mie sijawahi kukitumia sababu wana vifurushi vingi sana na ni nafuu hakuna mtandao unaofikia TTCL kwa unafuu wa vifurushi vyote ikiwemo vya data.
Tangu nijiunge ttcl sijawahi hama, hasa kwenye data.
 
Nzuri sana iyo, vipi kuhusu vufurushi vya data.
Hatua za kuboresha huduma zetu zinaendelea kufanyika ili kuwapatia wateja wetu huduma iliyobora.Kuhusu watendaji wetu,tumelipokea na tutachukua hatua.
Kwetu sisi mteja ni mfalme.
 
TTCL wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye soko kama safaricom ya kenya, ila sijui wanakwama wapi, wajiri wakurugenzi wenye uzoefu na uwezo kwenye telecom industry, haya mambo ya kuchaguana kikada kada ndio yanapelekea kushindwa kusonga mbele.
TTCL kwa namna ilivyo ni kama Tanzania ilivyo kama nchi ina rasilimali ya kila aina lakini bado tupo kwenye wimbi la umaskini.
Asante kwa kutuandikia.
Hatua za kuboresha huduma zetu zinaendelea kufanyika ili kuwapatia wateja wetu huduma iliyobora.Kuhusu watendaji wetu,tumelipokea na tutachukua hatua.
Kwetu sisi mteja ni mfalme.
 
Acheni utani jamani! Yani elfu 5 mb500 na dk 300? Kweli?

Wakati halotel hapo unapata gb10 na madakika karibu elfu 2?
Hatua za kuboresha huduma zetu zinaendelea kufanyika ili kuwapatia wateja wetu huduma iliyo bora.
Asante kwa kuchagua TTCL

Rudi Nyumbani Kumenoga.
 
Sisi wa Ushagoo line zenu tumeweka nyuma ya simu, mtandao unasoma H+ sometimes mpaka 4g nikiwasha data hata msg za WhatsApp kuingia shida. Boresheni huduma haswa kwa kuongeza minara huku ushagoo na vifurushi vyenye uafadhali.
Hatua za kuboresha huduma zetu zinaendelea kufanyika ili kuwapatia wateja wetu huduma iliyo bora.
Asante kwa kuchagua TTCL

Rudi Nyumbani Kumenoga.
 
Kwa hivyo vi mb's mnavyotoa wala hamjanishawishi kabisa ,maana siku hizi naweka vocha special kwa ajili ya bundle , sms na dakika sio ishu tena kwangu ,
Hatua za kuboresha huduma zetu zinaendelea kufanyika ili kuwapatia wateja wetu huduma iliyo bora.
Asante kwa kuchagua TTCL

Rudi Nyumbani Kumenoga.
 
Back
Top Bottom