TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Tunashukuru kwa kutuandikia.
 
Cha kusikitisha wanamiliki 49% Airtel- sasa unaachaje kwako uanze kudandia kwa watu?
 
Usithubutu kutumia T pesa utakuja kulia... Wamepoteza tsh 50k zangu kizembe sana wakati nalipa bill... Mpaka leo hela imepotea hewani na hakuna msaada wowote wanatoa

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana kwa changamoto.
Naomba ututimie namba yako uliyofanya muamala na risiti ya muamala kwa msaada zaidi.
 
Wakati mwingine sipati notification ya bando kuja kuisha na kunisababishia usumbufu maana nategemea intaneti yenu kwa shughuli zangu.

Juzi nimeenda Tabata Kisukuru hakukuwa na mtandao imara kiasi kwamba huwezi kutumia intaneti.
 
Mtandao mzuri ila rekebisha yafuatayo:

1 Kuangalia salio la kifurushi unganisha vipengele vyote yaani mtu anaponunua kifurushi cha data, airtime na sms anapotaka kujua salio mtumie sms moja inayoeleza salio la data, airtime na sms badala ya Kuangalia kila kipengele peke yake.

2. Ongeza options kwenye vifurushi ili kumpa mteja uhuru zaidi wa kuchagua.
Kazi njema
 
I think TTCL ndio kampuni ya Serikali ambayo haijali watu wake wa chini kabisa,

Wanafunzi wana kifurushi Chao cha unafuu

Wafanyakazi wana kifurushi chao cha unafuu

But wale watu wa chini kabisa wakulima na watu ambao hawana kazi hawana kifurushi chao cha nafuu

Yaani mfano: mfanyakazi na mwanafunzi wanaweza kulipa Elf moja wakapata Gb1 but mtu ambae sio mfanyakazi wala mwanafunzi akilipa hiyo Elf 1 anapata 500M
 
Dodoma pale katikati ya mji mmerekebisha Internet? Mwaka jana ilikuwa chini sana mpaka inakera...
 
1. Poor customer service ( ham respond kwa wakati inaweza chukua hata lisaa sim zenu zinaita na hazipokelewe )

2. T pesa watoa huduma ndio hawajui wanachokifanya nilishawahi nunua kifurushi kupitia tpesa mpaka leo sikuwahi kuona kifurush nilichonunua kama miez 2 imepita.

3 Internet yenu sasa ivi kama inazidiwa mara yakwanza wateja walipokuwa wachache kifurush cha toboa night speed nikubwa sasa ivi ukijiunga mpaka uamke saa 10 au 11 asubuhi ndio kidogo utafanya mambo mawili matatu

swali.
Ivi hao watoa huduma wenu wanafanya kazi masaa 12 au vipi maana ukipiga simu zenu usiku ndio hata hakuna anayetaka kuipokea
 
Huduma zenu na kasi yenu nimeipenda na hongereni sana, Binafsi mimi kama mteja wenu sina changamoto ila nina pendekezo moja: nalo ni kuhusu kifurushi cha Tam tam kilichopo T-Pesa, mkilete kwenye menu ya kawaida pia
#Nyumbanikumenoga
Waweke kwenye menu ya kawaida ili usitumie T-pesa?
 
Kuna mdau amechangia vema sana hapo juu,
Changamoto kubwa ni hizi.
1.Network mbovu, sijui bandwidth yenu ni ngapi , wakati nyie ndo mna fiber optic.
2. Msg capacity , hapa mnakera sana, na mnasababisha nagombana na watu, msg zinafeli bila sababu .
3. Vifurushi vyenu vya watumishi hasa kile cha wiki, hakiko realistic , msg 200 kwa wiki ni chache sana, dakika pia, upande wa internet ndo balaa.?
4. Network stability pia ni tatizo
5. Huduma kwa wateja sio kabisa, hampokei simu kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…