TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Natumia TTCL laini mwaka sasa. Kero zangu ni hizi hapa:

1. Menu ya TTCL ya kuangalia salio la bando ni ya kidwanzi kuliko udwanzi wenyewe. Yaani unaingia menu, unabonyeza kuangalia salio, HAFU ETI ANATOKEA SUB MENU ANAKUULIZA SALIO LA SMS, DAKIKA, AU MB, unajifanya fala unabonyeza dakika, ANATOKEA TENA ANAKUULIZA DAKIKA ZA TTCL KWENDA TTCL AU KWENDA MITANDAO MINGINE??????? SERIOUS??????????

2. Vifurushi vya SMS wamevibana sana. Mfano Chat Kijanja ndio ninao jiunga eti Buku 1 unapata SMS 1000 kwa week. Hakuna vifurishi vya SMS unlimited. Igeni kwa wenzenu.

3. Internet ikifika usiku haina kasi kabisa. Yes tunajua ni peak hours kila mtu yupo Quarantine kwake anatumia ila kwenu too much inaelekea kuna kitu mnabinya.

4. TTCL anzisheni App ya T-Pesa.

Kama wameshataja wadau hayo sorry ila mengine wataongeza wakuu.
Tunashukuru kwa kutuandikia.
 
Hivi vocha za TTCL wanatengeneza na madini gani?

Mbona kuzipata imekuwa taabu sana, yaani vocha kupatikana mtaani ni habari ya kushangaza.

Nyie TTCL kama kampuni mama ya mawasiliano nchini mnataka kufanya biashara au huduma? Nauliza kwa sababu hamuonekani katika biashara na katika huduma pia hampo.

Huduma zenu TTCL zinapatikana katikati ya miji kwa kiwango kizuri kidogo vipi huku mashambani au mtandao wenu ni kwa ajili ya watu wa mjini sisi wa mashambani tuendelee kutumia Buzz.

Kwanini TTCL msijitokeze nje ya ofisi mjitangaze watu wawajue nini mnafanya, naona kama mmejifungia ndani na promotion zikifanyika mitandaoni tu.

Ni mara chache sana mashirika ya umma kutoa huduma zenye kukidhi vigezo vya watumiaji kutokana na kubweteka ila najua mngekuwa na mikakati mizuri basi kila mtaa ungekuwa unaimba TTCL katika mtazamo chanya ila kelele za sasa ni malalamiko ya huduma, hii inadhihirisha kuwa bado hamna mikakati kabambe ya kuteka sekta ya mawasiliano nchini huwenda tuwape miaka mingi.
Cha kusikitisha wanamiliki 49% Airtel- sasa unaachaje kwako uanze kudandia kwa watu?
 
Habari ya jioni,

Ndugu mteja tunaomba utufahamishe changamoto unayoipata pindi umapotumia mtandao wetu wa TTCL.

MUHIMU
1. Kumbuka kutaja eneo ulilopo.
2. Aina ya tatizo.

NB: Kama una mapendekezo ya vifurushi na pia maoni kuhusu huduma zetu unakaribishwa.

Rudi Nyumbani Kumenoga.

27972579_10156214725942884_628791185432770219_n.jpg
 
Wakati mwingine sipati notification ya bando kuja kuisha na kunisababishia usumbufu maana nategemea intaneti yenu kwa shughuli zangu.

Juzi nimeenda Tabata Kisukuru hakukuwa na mtandao imara kiasi kwamba huwezi kutumia intaneti.
 
Mtandao mzuri ila rekebisha yafuatayo:

1 Kuangalia salio la kifurushi unganisha vipengele vyote yaani mtu anaponunua kifurushi cha data, airtime na sms anapotaka kujua salio mtumie sms moja inayoeleza salio la data, airtime na sms badala ya Kuangalia kila kipengele peke yake.

2. Ongeza options kwenye vifurushi ili kumpa mteja uhuru zaidi wa kuchagua.
Kazi njema
 
I think TTCL ndio kampuni ya Serikali ambayo haijali watu wake wa chini kabisa,

Wanafunzi wana kifurushi Chao cha unafuu

Wafanyakazi wana kifurushi chao cha unafuu

But wale watu wa chini kabisa wakulima na watu ambao hawana kazi hawana kifurushi chao cha nafuu

Yaani mfano: mfanyakazi na mwanafunzi wanaweza kulipa Elf moja wakapata Gb1 but mtu ambae sio mfanyakazi wala mwanafunzi akilipa hiyo Elf 1 anapata 500M
 
Dodoma pale katikati ya mji mmerekebisha Internet? Mwaka jana ilikuwa chini sana mpaka inakera...
 
1. Poor customer service ( ham respond kwa wakati inaweza chukua hata lisaa sim zenu zinaita na hazipokelewe )

2. T pesa watoa huduma ndio hawajui wanachokifanya nilishawahi nunua kifurushi kupitia tpesa mpaka leo sikuwahi kuona kifurush nilichonunua kama miez 2 imepita.

3 Internet yenu sasa ivi kama inazidiwa mara yakwanza wateja walipokuwa wachache kifurush cha toboa night speed nikubwa sasa ivi ukijiunga mpaka uamke saa 10 au 11 asubuhi ndio kidogo utafanya mambo mawili matatu

swali.
Ivi hao watoa huduma wenu wanafanya kazi masaa 12 au vipi maana ukipiga simu zenu usiku ndio hata hakuna anayetaka kuipokea
 
Huduma zenu na kasi yenu nimeipenda na hongereni sana, Binafsi mimi kama mteja wenu sina changamoto ila nina pendekezo moja: nalo ni kuhusu kifurushi cha Tam tam kilichopo T-Pesa, mkilete kwenye menu ya kawaida pia
#Nyumbanikumenoga
Waweke kwenye menu ya kawaida ili usitumie T-pesa?
 
Kuna mdau amechangia vema sana hapo juu,
Changamoto kubwa ni hizi.
1.Network mbovu, sijui bandwidth yenu ni ngapi , wakati nyie ndo mna fiber optic.
2. Msg capacity , hapa mnakera sana, na mnasababisha nagombana na watu, msg zinafeli bila sababu .
3. Vifurushi vyenu vya watumishi hasa kile cha wiki, hakiko realistic , msg 200 kwa wiki ni chache sana, dakika pia, upande wa internet ndo balaa.?
4. Network stability pia ni tatizo
5. Huduma kwa wateja sio kabisa, hampokei simu kabisa
 
Back
Top Bottom