TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Line yenu ntairudisha store, .
Vifurushi vyote mmevipindua pindua, sisi tukajua huu mtandao ni wa watanzania wanyonge tujivunie kurudi nyumbani kumbe ilikuwa geresha tu.

Juzi imefika SAA sita nimeweka vocha yangu natafuta toboa bando silioni daaah mipango kibao mliifelisha.

Nkabidi nikimbilie mtandao mwingine.
TTCL Corporation tunawatakia Waislamu na Watanzania wote Sikukuu njema ya Eid Al-Hajj
Furahia Sikukuu ukiwa na mtandao Bora, Nafuu na Salama.View attachment 1522469
 
Mmeharibu BOOM PACK bundle alaf mnakuja kujipigisha kelele humu.Nimewahama!
 
Nilikuwa naitafuta Toboa hapa. Naona wamenitoboa, 2500 kwa GB 9 wakati hapo ningepata GB 20+, mmekula ya mwisho hiyo mkuu. Yaani mnabadilisha vifurushi kienyeji tu. Hata mimi nawahama!
Siwezi kukesha bure leo!
 
Nipo DAR, Kawe Beach upeponi, sms zenu ni kero, mna support less than 160 characters
Tatizo kubwa upande wangu nanunua bando nikiwasha Data sipati chochote kutoka kwenye Internet wakati Gb Simon za kutosha nimefanya Settings zote vizuri lakini hakuna matokeo yake unatumiwa sms kua kifurushi kime kwisha wakati sijapata hata sms moja kutoka WhatsApp wala video au audio yenye uwezo wa mb 10 kutoka mtandaoni


Mimi nipo Gongo la Mboto
 
Mkuu, namba yako tafadhali
 
Yani mlianza Vizuri na slogan yenu”Rudi Nyumbani Kumenoga” Tumewapokea vizuri sasa mmelewa sifa. Kifurushi cha Boom Pack ni mahususi kwa wanafunzi. Bila taarifa wala kujali umuhimu wa kifurushi cha wanavyuo kimefutwa kilianza 1500 Mara 2000, Kutoka 2500-3500.Mmeshindwa kuiendesha hiyo biashara turudi ugenini? Mkataa kwao ni mtumwa. Ila itabidi tuukubali utumwa kufata unafuu na Huduma Bora.
 
Katika kosa kubwa nililowahi kufanya maishani mwangu ni kumiliki line ya TTCL Corporation.
Sms mwisho ni character 150.
Sms unatuma leo, inafika kesho.
Network sio ya uhakika
Usikivu mbovu.
Narudi zangu Tigo Tanzania.
Tigo mnisamehe, shetani ni mbaya, alinidanganya eti RUDI NYUMBANI KUMENOGA, badala ya kunirudisha nyumbani, akanipeleka pangoni.
Bye bye shetani, kuanzia leo nakukataa wewe na hila zako za urubunifu eti RUDI NYUMBANI KUMENOGA, wakati kumechacha hadi kumechalala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…