TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Threads gani afisa habari wa idara ya serikali aliwahi kujibu kwa wakati maswali ya wadau?

Yaani bajeti yao inaisha pale anapotoa andiko tu, maswali yakielekea kupewa majibu mpaka aombe bajeti ipitiwe apewe ndipo aje ajibu [emoji40]!.
Mambo ya posho[emoji38][emoji38][emoji38]
 
aghh, hayo mnayoyasema yapo TTCL ipi, maana niliyokuanayo mm bei zake zipo hivuo
 
Hakika kumenoga
Nilikuwa sivijui vifurushi vingi tu kumbe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mmekuwa mtandao wa hovyo kuliko hata nilivyo tegemea


Awali licha ya mapungufu yenu mliyonayo kama ya kutokuwa na branch za mawakala wa T-pesa sehemu nyingi tofauti na ilivyo kwa wapinzani wenu network ya mtandao wenu kutokuwa inasoma baadhi ya maeneo tena ya mjini kabisa


na vouchers zenu kutokuwa hazipatikani maeneo mengi Yote haya nilikuwa nayavumilia niliamua kurudi nyumbani na kujisemea kuwa kumenoga kama namna ambavyo mlivyo kuwa mmetuaminisha lakini baada ya kukutana na hizo changamoto tajwa katika hii comment nikawanina jipa moyo na kusema kwamba niwavumilie tu cuz nyumbani ni nyumbani hata kama nyumbani hapo patakuwa na baba mlevi au mama mzinzi sinto weza kupakana kuwa sio nyumbani still patabaki kuwa nyumbani na huyo baba mlevi /mama mzinzi siwezi kumtafutia mbadala still atabaki kuwa ni mzazi wangu tu

Ila sasa Hatua mliyofikia Imenikera sana Yaani sina hata hamu ya kuendelea kutumia Huu mtandao wenu kitendo cha kupandisha gharama za vifurushi tena vimekuwa ghari kuliko hata vifurushi vya makampuni mengine ya simu kimenishangaza sana '

yaani nyinyi ambao ndio kampuni mama ya taifa hili na kampuni ya wananchi mnaanzaje kuwa na vifurushi vyenye gharama kubwa kiasi hicho yaani badala ya kuwasaidia wananchi wanyonge ndio kwanza mnawakandamiza

Kama nyinyi ambao mmepewa dhamana ya kuhakikisha mnatatua changamoto za mawasiliano kwa raia wa Tanzania mnawafanyia hivyo watanzania hali itakuwa vipi kwa makampuni binafsi ""!??

Mnafeli sana aisee mmetufanya sisi tuliorudi nyumbani tukiamini kuwa kumenoga tupaone nyumbani kuwa ni ugenini tena Pana nuka harufu ya jehanamu

Huu mtandao wenu sinto diriki kuutumia tena ..
 
Kwa nn mmepandisha mambando yenu hvyo ya internet hamjui kwamba watu tunawahama maana tulikuwa tunatumia ttcl kwa ajili ya internet tu. Huo utafiti wenu mliofanya mkapandisha mabando ni wa uongo sana
Jamaa wamefeli sana ... Niliwakimbia tigo kwa sababu yao ...lakini Jana nilikuwa natizama menu ya tigo wamepunguza gharama ya vifurushi . wameweka vifurushi rafiki kabisa kwa maisha ya mtanzania ..... So naanza kutumia tena tigo rasmi baada ya hili likampuni la TTCL kujaa ukiritimba na ubabaishaji
 
Nataka kufahamu iwapo toboa night package imeondolewa au vipi?
 
Punguza jazba basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…