TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Bora umenena
 
Mm Dhana yangu
Hapa tunaongea na ROBOT

Tusiweke matarajio ya aina yoyote katika maoni au malalamiko yetu juu ya Wahusika hawa(ROBOT)
 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea Banda la TTCL katika kilele Cha maadhimisho ya maonesho ya NaneNane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu na kufurahishwa na ubunifu uliofanywa na TTCL wa kuanzisha mfumo wa T- HAKIKI unaolenga kuwakomboa Wakulima kuhakiki ubora wa pembejeo kupitia simu ya mkononi.
ASANTE WAZIRI MKUU!


TTCL yaibuka mshindi wa tatu wa jumla wa maonesho ya NaneNane Kitaifa na mshindi wa kwanza katika kipengele cha watoa huduma za Mawasiliano nchini.
Rudi Nyumbani Kumenoga!
#NaneNaneSimiyu




Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Elias John Kwandikwa akiangalia bidhaa zinazotolewa na TTCL alipotembelea Banda la TTCL katika maonesho yanayoendelea ya Wakulima (NaneNane) katika Viwanja vya Nyankabindi mkoani Simiyu.


Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga amezindua huduma maalum ya kuhakiki pembejeo inayojulikana kwa jina la T-HAKIKI huduma itakayomwezesha mkulima kuhakiki ubora na matumizi sahihi ya pembejeo kupitia simu ya mkononi. Rudi Nyumbani Kumenoga!






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan atembelea Banda la TTCL Corporation katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
#Rudinyumbanikumenoga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…