TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Mnazingua Sana, vifurushi vya data viko bei juu kuliko hata makampuni mnayoyauzia.
Pia mmeondoa kifirushi cha wiki cha 1.5 gb kwa buku, ili mtunyonye vizuri then mtoe gawio

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
Hii ndo ajabu inayonichoshaga , wanawauzia wenzao alafu wenzao wanaenda kuuza bei ndogo kuliko walio wauzia, hayo ni makodi ya umma
Hawajui kuweka wabunifu, yaani nyie
TTCL bado sana mna boa
 
Hongereni sana TTCL

Kweli mmejitahidi sana lakini bado mna uwezo wa kufanya vitu vikubwa zaidi kama kampuni mama ya kitanzania.

Nyie pamoja na mashirika mengi ya umma mmekua na mazingira yote mazuri katika kuweza kumfikia kila mtanzania, kwenye kutoa huduma bora, kwenye kuboresha huduma kwa watumishi wake ila SHIDA KUBWA IMEKUA KUENDELEZA NA KULINDA MIUNDO MBINU PAMOJA HUDUMA KWA WALAJI.

TTCL TTCL Customer Care mnatakiwa kubadilika sana kwenye customer care yenu. Wateja wenu wawe ni makampuni au ni watanzania wa kawaida hamuwajali wateja kivilee, mara nyingi majibu tunayopewa tunapohitaji huduma tunakata tamaa na kuishia kwenda kwa kampuni zingine. Mnatakiwa kuijua tabia ya soko, soko la watanzania ukilijua utawauzia kila kitu

Ushauri kwenu punguzeni URASIMU, angalie vitu visivyo muhimu kwenye mifumo yenu ya kitandani mviondoe, boresheni utendaji wa wafanyakazi wenu kwa kuwakwekea mfumo wa kuwapima na kuwapa motisha kadri ya utendaji wao ili kuikuza kampuni yenu na kuongeza faida. Tuko kwenye ulimwengu wa ushindani mkubwa kibiashara kibiashara msipobadilika tutaendelea kutumia vya wageni na kuwapa faida kwa asilimia kubwa huku vyetu vikisuasua
 
Asante sana mama D kwa ushauri wako.
Tumeupokea na tunaufanyia kazi.

#RudiNyumbaniKumenoga
 
Nataka kuwa wakala wenu wa kusajili lain na kutoa pesa nafanyeje ndugu
Asante sana ndugu nurman kwa kuwasiliana na sisi.
Ili kuwa wakala wa T PESA, vifuatavyo ni vitu vinavyohitajika ili uwe wakala na msajili laini
1. Kitambulisho cha uraia/kura/leseni/pasipoti ya kusafiria.
2. Leseni ya biashara pamoja na TIN namba ya biashara.
3. Mtaji ambao kianzio ni Tsh 50,000/=

Hivi ndo vitu vya muhimu maelekezo mengine utayapata ofisini.

#RudiNyumbaniKumenoga
 
Tafadhali naomba bei za wi-fi? Nina ofisi Dar na Arusha
Asante kwa kuwasiliana nasi.
Ndugu mbongopopo, inategemea unahitaji WiFi ya aina ipi?
Maana tuna
1. Dongle hii moden ya kawaida Tsh 50,000/= inatumia mtu mmoja tu.

2. Wingle Tsh 75,000/= inatoa wifi kwa watu 10.

3. Mifi Tsh 110,000/= inatoa wifi kwa watu 10.

4. Router Tsh 150,000/= inatoa wifi kwa watu 32.

Karibu sana.

#RudiNyumbaniKumenoga.
 
TTCL mmejitahidi ila speed yenu ya internet ni ndogo mno,, kwa mtu ambaye upo busy na mambo mengi huwezi kuvumilia lazima atawakimbia aende kwa provider wengine,,

Jaribuni kulifanyia kazi hili, nmeona watu wengi tu wanalalamika, mimi ni mhanga wa hilo pia! Nilichukua bando lenu sikuweza kutumia kwa sababu ya speed kuwa ndogo nikarudi kwa provider wengine!!
 
Adi Ninaondoka kwenye uso wa Dunia sijuwi kama Nina weza juwa kwanini mlikubali kurudi chini wakati mlikuwa na mtandao nchi nzima!!
Kuna watu ilibidi wanyongwa kama Mangu angeweza nyonga walio dhoofisha ilo shirika tungempa miaka 20
 
Hakika nyumbani kumenoga, mna huduma nzuri sana hongereni
 
Asante sana kwa ushauri wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…