Hongereni sana TTCL
Kweli mmejitahidi sana lakini bado mna uwezo wa kufanya vitu vikubwa zaidi kama kampuni mama ya kitanzania.
Nyie pamoja na mashirika mengi ya umma mmekua na mazingira yote mazuri katika kuweza kumfikia kila mtanzania, kwenye kutoa huduma bora, kwenye kuboresha huduma kwa watumishi wake ila SHIDA KUBWA IMEKUA KUENDELEZA NA KULINDA MIUNDO MBINU PAMOJA HUDUMA KWA WALAJI.
TTCL
TTCL Customer Care mnatakiwa kubadilika sana kwenye customer care yenu. Wateja wenu wawe ni makampuni au ni watanzania wa kawaida hamuwajali wateja kivilee, mara nyingi majibu tunayopewa tunapohitaji huduma tunakata tamaa na kuishia kwenda kwa kampuni zingine. Mnatakiwa kuijua tabia ya soko, soko la watanzania ukilijua utawauzia kila kitu
Ushauri kwenu punguzeni URASIMU, angalie vitu visivyo muhimu kwenye mifumo yenu ya kitandani mviondoe, boresheni utendaji wa wafanyakazi wenu kwa kuwakwekea mfumo wa kuwapima na kuwapa motisha kadri ya utendaji wao ili kuikuza kampuni yenu na kuongeza faida. Tuko kwenye ulimwengu wa ushindani mkubwa kibiashara kibiashara msipobadilika tutaendelea kutumia vya wageni na kuwapa faida kwa asilimia kubwa huku vyetu vikisuasua