TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Badala ya kutumia muda mwingi kwa kujivunia.., tumieni huyo muda kubuni, kuboresha na kuendeleza.... Mkifanya hivyo wala hautahitaji kuwaambia / kuwakumbusha watu wenyewe watakuwa wanaambiana tu.... Kama wenye busara walivyosema Kizuri Chajiuza.....
 
Mimi binafsi sihaongeza Salio mwezi Sasa baada ya kupandisha 1500 gb1 hiyo Ni wizi, vifurushi vya chuo mmeobeza Bei, Bando tamtam mmefuta. Basi Bali na Ttcl yenu
 
Asante kwa ushauri wako.
Nitaufikisha kwa menejementi.

#RudiNyumbaniKumenoga
SIO NITAUFIKISHA KUA PROFFESIONAL..NI TUTAUFIKISHA....NA WEWE NDO KAMPUNI TUNAHITAJI MAJIBU YALIYOJITOSHELEZA....MNAISHI KWA MAZOEA..MAWAKALA WAMEJAA NJE YA JENGO LENU ILA HAMFUATI RAIA WALIPO...KWENYE MFUMO WA SIMU ZA MKONONI MMEFERI KWA KWELI
 
Rekebisheni kifurushi cha bandika bandua, angalau iwe GB 1 saa mchana na GB 3 usiku mwa manane. Mkifanya hivyo mimi naachana na halotel. MB 500 mchana ni ndogo,
 
Hongera sana TTCL kazi yenu iko wazi kila mpenda maendeleo anaona wazi.
Rekebisheni bei za vifurushi angalau muendane na airtel hayo ni mawazo yangu
ubora uendane na nguvu ya mnunuaji itapendeza zaidi.
 
Waongo wakubwa nyie

Vocha tu haipatikani,t.pesa ni ujinga ujinga tu unatoa pesa haitoki au unatuma haiendi kila siku network mbovu,mbaya zaidi hakuna mawakala wa kutosha wa T.pesa!!


Maajabu mengine kwamba mmefanya biashara mkapiga faida kiasi mkajikuta mnatoa gawio la 3.6 billion kwa biashara ipi mnayopiga faida kiasi hicho?


Boresheni huduma naimani mna mtaji kwa sababu mnajiendesha kwa kodi za watanzania!
 
Niliwahi kumsikiliza Prof Lumumba,akisema "ukifanya kitu,harafu ukatumia muda mrefu kueleza ulichofanya,badala ya kuacha ulichofanya kijitsngaze,Basi ujue hujafanya kitu"
TTCL,imehujumiwa sana,watendaji wakuu wote ilibidi wawe jela.
Kwanza tuanze,TTCL ina data center ngapi?Tigo wanazo tatu ambazo ni Tier three,kiwango Cha kimataifa.
Nenda kwenye tower za TTCL uone Miundombinu ilivyo chakaa,TTCL Wana switch ngapi?nenda mbezi juu,uone switch ya Voda,ilivyo ya kiwango Cha juu.
Ili shirika,wanaoliongoza Wana vikampuni vidogo,kiasi kwamba Kuna mgongano wa kimaslahi mkubwa.
Sasa hv,hata ukitembea dar,uwezi kusikia inaitwa njoo usajiri au ununue laini ya TTCL,utasikia Voda,Tigo,halotel,
Kazi kubwa inahitajika.
Sio hizi mbwembwe.
Kama vp,tafuteni management kutoka MTN sothafrica.
 
Sawa mkuu, tumekusikia.
 
Kwa kifupi kabisa,kajifunzeni Voda,Tigo,Halotel na Airtel wanachofanya,nyie bado mpo nyuma sana kiasi tunaogopa hata kujiunga na nyinyi,vocha zenu hazipatikani,mawakala wenu hakuna,yani unazunguka mjini kuitafuta TTCL huipati,nadhani bado mpo nyuma sana.
 

Kujifunza toka kwa washindani wao Voda,Tigo,Halotel na Airtel ni moja. Mbili ni kuboresha zaidi na kuweka utofauti kati ya TTCL na hao wengine. Hii inawezekana sana na wakiweza hilo watakua juu mawinguni
 
Ndugu ttcl.
Ulishawahi kusikia sukari ya Kilombero inapigiwa debe kwamba Ni tamu?
Huu muda mnaotumia kusema blah blah, mngekua mnaotumia ku upgrade mitambo, huduma na watanyakazi. Kuna tofauti kubwa sana Kati ya mfanyakazi wa Vodacom na wa TTCL. Utafikiri wa TTCL anajitolea
 
Ndiyo bado ninayo
Nbona simpo tu mkuu.
Ingia SETTING kisha sehemu ya SECURITY.
Baada ya hapo,angalia walipoandika SET UP SIM CARD angalia ipo laini ya TTCL kama ipo ON weka OFF kisha ingiza PIN zilizopo kwenye kikadi cha laini.
 
[emoji51][emoji51][emoji51][emoji51] ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…