TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Tumekurahisishia! Sasa nunua kifurushi chako pendwa cha BUFEE na ulipie kupitia akaunti yako ya T PESA.
Ni rahisi sana.
Piga *148*30#
Kisha ingiza 6 BUFEE PACK
Jitengenezee kifurushi kisha chagua lipa kupitia T PESA.

#RudiNyumbaniKumenoga
View attachment 2140707
Hii huduma ni gumashi haipo kwani ukinujua bufee kwa t.pesa hupati kifurushi na pesa hairudi.


Mimi tangu tarehe 25.02.2022 nimenujua bufee ya 10,000 kwa t.pesa sijapata kifurushi na hao huduma kwa wateja ndiyo pumbafu kabisa hamna wanachojua
 
Tangu tarehe 18 mwezi huu mmenikata 1704 lkn sikupata data Wala dakika, nimepiga simu zaidi ya Mara 6 lkn sipati msaada, Ttcl acheni wizi na utapeli nataka hela yangu
 
1500/= ni SMS 2000 tu aiiii ongezeni SMS.

Mitandao mingine 1000/= unapata SMS 6000.

Ushauri, ongezeni idadi ya SMS kwa 1500/= mtu apate hata SMS 5000.
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (T-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)

- Maeneo gani? (Tukifahamu maana ulipo, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate msaada toka kwa wakala wetu aliye karibu nawe)

- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?

- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza.

- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.


Zifuatazo ni ofisi zetu za huduma kwa wateja ndani ya jiji la Dar es Salaam.


1. POSTA
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Samora, jengo la Extelecom ghorofa la Chini.


2. KARIAKOO
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Makamba/Msimbazi, jengo la Akamba Bus Service.

3. UPANGA
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Magole/Maliki, karibu na Diamond Jubilee.


4. MAGOMENI
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Minaki/Fundiki, karibu na Manispaa ya Kinondoni.


5. KIJITONYAMA
[emoji654][emoji654][emoji654]Kijitonyama Sayansi, barabara ya Ali Hassan Mwinyi/ Rose Garden.


6. OYSTERBAY
[emoji654][emoji654][emoji654]Barabara ya Haile Selassie.


7. UBUNGO
[emoji654][emoji654][emoji654]Jengo la Ubungo Plaza/ Ghorofa la chini.


8. MBEZI BEACH
[emoji654][emoji654][emoji654]Mbezi Makonde/ Jengo la Shamo Tower.


9. TABATA
[emoji654][emoji654][emoji654]Tabata Bima, barabara ya Segerea karibu na kanisa la Romani Katoliki.


10. CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.
[emoji654][emoji654][emoji654]Jirani na tawi la benki ya NBC, jirani na kilipo kituo cha polisi cha UDSM.


11. BARABARA YA PUGU
[emoji654][emoji654][emoji654]Barabara ya Mwalimu Nyerere, karibu na Sigara.


12. WAGENI
[emoji654][emoji654][emoji654]Uwanja wa ndege.


13. PUGU
[emoji654][emoji654][emoji654]Jengo la Quality Centre, ghorofa la chini.


14. KISUTU
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Mchafukoge/Libya jengo la Haad Plaza.


15. TEGETA SHOP
[emoji654][emoji654][emoji654]Jengo la Kibo Complex, ghorofa la chini.


16. MWANANYAMALA SHOP
[emoji654][emoji654][emoji654]Mwananyamala A, barabara ya Mwinjuma yalipo makutano ya Mwananyamala A.


17. KURASINI
[emoji654][emoji654][emoji654]Kurasini Exchange Area, jirani na Chuo cha Diplomasia.


Wasiliana nasi:
[emoji337]022 210 0100
[emoji390] 0738 151 511
[emoji273]www.ttcl.co.tz


#RudiNyumbaniKumenoga
View attachment 1529645


Karibu.

Rudi Nyumbani Kumenoga
Tumeomba kuunganishiwa huduma ya internet tokea mwezi wa 08 mwaka jana hadi leo hatujafanikiwa kuungiwa , shida ni nn
 
Huu mtandao uko kizamani, haukubali kuingia menu yoyote ya bank.
 
Back
Top Bottom