A
Toka aondoke Kindamba akapelekwa mwendo Kasi hii kampuni imeshaanza kuishiwa pawaKumekuwa na changamoto ya ajira kwenye kampuni ya TTCL kwa zaidi ya miaka 3 sasa. Watu wanafanya sana kazi za internship bila kuajiriwa. Pia mikataba yao siyo mizuri; kwa zaidi ya miaka sasa intern wanalipwa tu posho, lakini hawana ajira za kudumu. Pia hawana bima wala NSSF.
Watu wanaambiwa shirika halina hela, hivyo wavumilie wataajiriwa, lakini wanafukuzwa mwisho wa siku. Hawa watu wataenda wapi? Mtu ameifanyia kazi kampuni miaka lakini hapati ajira. Tunaomba Wizara ya Kazi iingilie kati hili suala.
Watu waajiriwe wanaostahili ni wengi, lakini watu hawapati ajira, na wafanyakazi wakifukuzwa wanaanza kuteseka mtaani kutafuta ajira wakati kampuni imeshindwa kuajiri. Sio haki. Pia mameneja wa mikoa wachunguzwe; baadhi yao ni wanyanyasaji mikoani, wanatesa vibarua wao na kujiona miungu watu.
Pia baadhi ya mikoa ichunguzwe, Tabora na Mtwara; unyanyasaji ni mkubwa.
Wabongo tuache kukariri bila kutafakari. Si kila ajira ya serikali inapaswa kupita Sekretarieti ya Ajira. Yapọ mashirika ya kibiashara ya umma ambayo yamepewa uhuru wa kutafuta na kuajiri rasilimali watu bora kulingana na mahitaji yao, kwa lengo la kuongeza ufanisi, ushindani na ukuaji wa taasisi husika. Kauli nyingine tunapozitoa zinaonyesha wazi kuwa bado tunafikiri kwa mtazamo wa zamani usioendana na mazingira ya sasa ya maendeleo.Ajira za Serikali zinatolewa na Sekritariati ya ajira
sio ttcl tu bali mirad yote ya serikal imefer kbsKuna vitu vinachekesha sana yaan ttcl ikuajir wewe wakat wao hata kuuza tu vocha huku mtaan wameshindwa kabisa
N shirika.ambalo linategemea kudra za serikal (gawio) ili lijiendeshe