HOJA TTCL inapaswa kuboresha utoaji wa taarifa kwa wateja kuhusu huduma zake za intaneti

HOJA TTCL inapaswa kuboresha utoaji wa taarifa kwa wateja kuhusu huduma zake za intaneti

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

bawazir

New Member
Joined
May 11, 2010
Posts
1
Reaction score
0
TTCL inapaswa kuboresha utoaji wa taarifa kwa wateja kuhusu huduma zake za intaneti. Kwa sasa, hakuna taarifa zinapotokea hitilafu za huduma, huduma zinaporejea, au kunapokuwa na matengenezo yaliyopangwa (scheduled maintenance).

Hii ni changamoto ya muda mrefu ambayo imekuwa ikiwasababishia usumbufu wateja wengi, hasa wale wanaotegemea intaneti kwa shughuli za kazi na biashara.

Tunashauri TTCL itumie kurasa zake za mitandao ya kijamii pamoja na ujumbe mfupi wa simu (SMS) kuwataarifu wateja kuhusu hitilafu, matengenezo yaliyopangwa na kurejea kwa huduma, ili kuwawezesha kupanga shughuli zao ipasavyo.
 
hicho ni kichwa cha wendawazimu, taasisi mbovu sana ya mawasiliano nchini wanachoweza zaidi ni kupaka rangi ofisi zao.
 
Back
Top Bottom