A
Anonymous
Guest
Naandika hoja hii nikiwa mwananchi na Mkazi wa Kijiji cha Nyambili, Tarafa ya Bungu, Wilaya ya Kibiti, Mkoani Pwani kuna kero inayotukabili tangu mwaka 2020 hadi leo bila kupata ufumbuzi wala haki yetu.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) lilikuja na kujenga mnara wa mawasiliano katikati ya shamba letu la familia. Hata hivyo, mchakato mzima wa uchukuaji wa eneo hili ulitawaliwa na ukiukwaji mkubwa wa haki.
TTCL hawajawahi kuja kuzungumza na sisi wamiliki halali wa eneo, baada ya kuona kuwa kuna mawimbi (signal) mazuri eneo letu, walienda serikali ya kijiji kuomba eneo.
Viongozi wa kijiji walimtafuta ndugu yetu mmoja (ambaye hakuwa mmiliki wala hakuwa na uelewa wa kisheria), wakamshinikiza kusaini mkataba/muktasari wa kijiji kwa niaba yetu bila sisi wenyewe kutambua wala kushirikishwa.
Wakati wa ujenzi wa mnara huo, TTCL waliharibu vibaya mazao yetu ya kutoa kipato ikiwemo mikorosho na miembe, pamoja na kuchimba shimo kubwa sana ambalo hadi leo wameacha wazi bila kufukia, jambo linalotishia usalama wetu.
Hadi leo hatujalipwa hata senti moja kama fidia ya eneo wala mazao yaliyoharibiwa. TTCL wanadai kuwa serikali au wao kama shirika la umma "hawalipi eneo na wanachukua bure".
Tumefuatilia kero hii katika ngazi zote za uongozi hadi kufika kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti. Cha kusikitisha, Mkuu wa Wilaya naye alitujibu kuwa "TTCL ni ya serikali hivyo hawezi kuwalazimisha kulipa eneo," na badala yake akatuambia kama hatujaridhika twende mahakamani tukatake madai wetu!
Kijijini kwetu tunashindwa kuelewa; Kijiji kinasema hakijapokea malipo, Mkuu wa Wilaya anasema hawalipi, na sisi wenyewe hatujapewa fidia yoyote wakati eneo letu limetwaliwa na mazao yetu kuangamizwa. Tunahisi kuna watu au viongozi wa pembeni wanajinufaisha na mradi huu huku sisi wamiliki wa ardhi tukiachwa tukiumia.
Tunamwomba Mheshimiwa Rais, Mawaziri husika, na Mamlaka za Juu za Serikali kuingilia kati swala hili. Hivi ni utaratibu gani unaoruhusu shirika la umma kuchukua ardhi ya mwananchi kwa nguvu, kuharibu miundombinu na mazao ya miaka mingi, kisha kukataa kutoa fidia kwa kisingizio cha kuwa "serikali hailipi ardhi"? Tunaomba msukumo wa viongozi wa juu ili tupate haki na fidia zetu zinazostahili.
Ufafanuzi wa Shirikika ~ TTCL yafafanua hoja ya kuweka mnara Kibiti kisha kutoilipa familia husika