Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,101
Tanzania kama nchi hatupigi hatua yoyote kwenye soka la upinzani. Si kwa Afrika Mashariki(CECAFA), sio Afrika(CAF), wala dunia(FIFA)
Tunazidi kujidanganya kua pengine kesho mambo yatakua mazuri, sijui tupeane muda hususan kuwapa muda makocha na blahblah kibao
Mwaka hadi mwaka viwango(quality) ya wachezaji wa Kibongo inazidi kupungua. Hata hizi "Soccer Academy" zinazofunguliwa haziwezi kua muarobaini wa kupata wachezaji wenye vipaji
Mifano ipo mingi. Tuangalie records za vijana wetu waliokua wanaibuka miaka tofauti kuanzia wale walioingia fainali ya Coca Cola World Cup, timu zetu za under 17 na under 20 wanakoishia! Wakitoka hapo kwakua "hawaujui" mpira na mpira "hauwajui" hawana wanapokwenda, si ndani wala nje ya nchi
Dawa sasa hivi naona ni kurudi kwenye soka letu la asili. Soka ambalo ilikua ni burudani kwenda uwanjani. Burudani kuona vipaji vya asili kabisa kama vya kina Selestine "Sikinde" Mbunga, Nico Njohole, Hamis Thobias Gaga na wengi wengine. Soka la akina Abdallah Kilewo wa Mwananyamala na wengine wengi waliokua wakikusanya watu viwanjani waone burudani iliyokamilika
Inawezekana hawa jamaa(vizazi vya wanasoka vilivyopita) hawakufanya vizuri kimataifa lakini unaona ni kwavile walikosa mechi nyingi na timu za nje ili wapate exposure kidogo tu na wafanye makubwa. Miaka ile unaenda uwanjani kuangalia kiungo fulani au beki fulani anavyonyumbulika na mpira au mshambuliaji mwenye sifa zote za ushambuliaji
Wakati huo ukiwa Mwanza hutataka kukosa mechi ya Pamba, ukiwa Moshi utahakikisha unawaona Ushirika au kule Songea Majimaji nk
Kinacho tuponza sasa ni mafunzo ya mpira yanayoendeshwa na "takwimu". Eti kipa ana clean shit ngapi, kiungo/mshambuliaji ana assits ngapi na mambo kama hayo huku tumesahau kabisa suala la mchezaji kujua kuuchezea mpira(control). Kwanini hatuachi watoto wachezee mpira kama burudani badala ya kuwajaza na falsafa za kuigiza za soka la Ulaya lisilokua na ladha kama kuku wa broiler!?
Brazil nao ni wahanga wa mfumo unaoitwa wa kisasa wa mpira. Sasa hivi soka lao halivutii tena na wanapoteza mashabiki kwa kasi. Eti sasa hivi utaona mchezaji wa timu ya Taifa ya Brazil control inamsumbu!!! Watu wamekua wakilihusudu soka la Brazil na Amerika ya Kusini kwa ule udambwidambwi wao kupelekea hata Ulaya wakawahitaji wachezaji kutoka huko
Kizazi cha kina Jayjay Okocha Nigeria nacho ni zao la soka la mtaani ambapo vijana huachwa wachezee mpira watakavyo kuliko kuwabana na mbinu za kutaka ushindi tu! Na wao walipofungua Soccer Academy kwa wingi ili wapate pesa za kuuza wachezaji ni kama vile vipajo halisi vinapotea kwa kasi kwa kuminywa na mafunzo ya soka la "kitakwimutakwimu". Cameroon na kwengineko ni hivyohivyo
Kwa sasa hivi kama uwanjani timu zikitoka suluhu ya bila kufungana huna zaidi cha kukumbuka kwenye mechi hiyo. Mpira hauna ladha kabisaaaaa!
Kuna hatari miaka ijayo huko watu wataacha kupenda soka kwa maana ya kufurahishwa na mchezo kama burudani bali utabakia kama sehemu ya watu kuchezea kamari(betting)
Zamani ukienda kwenye mechi za mchangani akiingia mchezaji wa ligi kuu au hata daraja la kwanza utaona tofauti tu bila hata kuambiwa. Sasa hivi mchezaji wa ligi kuu hana tofauti na wa madaraja mengine
Tuchukue hatua angalau kama hatuwezi kushindana nje ya nchi basi tubaki na utamu wa soka letu lenye wach3zaji wenye uwezo wa kumiliki mpira(control halisi), kupiga vyenga na kanzu(shibobo) na udambwidabwi mwingine, maana mpira ni sanaa ya kufurahisha watu pia