Tuache kujichubua

Dejane

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
50,587
Reaction score
71,492


Ngozi inaharibika sanaa ukizeeka pia Mbona kuna wabibi wana ngozi nzuri sanaa na wamezeeka tuache kutumia vipodozi vikali

Mwanaume atakupenda tu hata ukiwa wa njano au mwekundu ukiona hajakupenda jua sio wako ,wako yupo tu atapenda rangi yako maana wanawake wengi wanahangaika kujipodoa sababu ya wanaume
 
Airport Dar (Julius Nyerere International Airport) kila siku Wachina hushuka na Wake zao lakini huwezipata Ke wa kichina wamefungasha maumbile bandia ya miili wasiwe kimbaumbau kiasilia kuliko Ke wa Bongo wasivyojiamini kwa uzuri wa maumbile yao ya asili hadi kulazimisha kuwa na;

✓ Matako na hispsi feki/bandia tokana na;

* Kupaka dawa.

* Kuchoma sindano za kuumua sehemu hizo.

* Kumeza vidonge.

* Kufanyiwa plastic surgery.

✓ Wigi (nywele za maiti).

✓ Kujichora chora mitatuu mwilini.

✓ Kujiwekea mipini puani kama ng'ombe.

✓ Kujiwekea mikope bandia.

✓ Kujiwekea mikucha mireeefu hadi ashindwe kujichamba chooni.

✓ Kupakaa rangi nyekundu kwenye lipsi za midomoni kama katoka kunywa damu ya Mtu.

✓ Kuvaa skin tights za vigodoro kujaladia hispsi na matako bandia.

MADHARA:

1. Nyeti za miili (K) kuwa na maji mengi, ubaridi.

2. Kansa za kizazi, damu, ngozi n.k.

3. Ke kupoteza hamu ya kujamiiana na mwenzi.

4. Ke kuzeeka na kukongoroka mapema kwa mbabuko wa ngozi na makalio kushuka.

Bongo tunakwama wapi?
 
Wana harufu fulani watu wanayotumia hayo madude hawajui tu haswa manywele yananuka , sometimes unakuta binti anajikuna Kuna machawa kibao wengine hawazioshi kabis hata mwezi
 
Halafu tukisemwa kwa kukosa akili na maarifa tunakuwa wakali. Waafrika tuna tatizo mahali, ama tunawekeza kwa vitu visivyo na maana.

Mtu unaenda kurefusha uume, kupaka mkongo, ili ugundue nini, unawekeza kwenye vitu vya kipumbavu, shukuru vile Mungu kakuumba endelea kuishi na kutimiza jukumu uliloitiwa duniani.

Waafrika wengi wetu hatujui purpose ya kuwepo duniani, tupo tu..ndio maana tunafanya mambo yasiyo na tija.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…