Tuache kuleta siasa kwenye soka, hatutafika popote

VYEMELO

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2020
Posts
349
Reaction score
464
Kuna ndugu alituonya Tanzania humu juu ya kuchanganya mchezo wa mpira wa miguu na siasa. Viongozi wetu badala ya kuwekeza kikamilifu kwenye mchezo huu maarufu, wanatafuta cheap political popularity kupitia soka. Modern Soccer is investment.

Ndugu ulitutabiria humu jana kufungwa na DRC, kweli tumefungwa. Wachezaji ktk soka la Dunia ya leo, wanatengenezwa. Hamna habari za ati Kipaji. Kipaji? Soka la leo siyo ndumba ndugu.

Mnadanganywa na "kamati za ufundi"? Hamna Football pattern niliyoiona kwa Taifa Stars leo ni kwamba Walikuwa wanajichezea. Nina hakika wachezaji hawakufuata wala kuzingatia maelekezo ya kocha. Na hili ni Tatizo la soka la Tanzania.

Sijui ni changamoto ya lugha kwa wachezaji wetu kwamba hawaelewani sawasawa na makocha? Sijui. Lakini pia, nilichokiona mechi hii ni changamoto ya kimo na nguvu. Wachezaji wa DRC wanaonekana kuwa warefu na wenye nguvu kuliko wetu. Aidha, DRC wameonesha proffessionalism kwa kucheza mchezo kwa kadiri ya maelekezo ya mwalimu wao.

Wamewaacha Stars watawale mchezo huku wakihakikisha nafasi chache wanazotengeneza wanazitumia vizuri kupata magoli. Na ndivyo ilivyotokea. Walitengeneza nafasi Nne, nafasi Tatu zikawa goals. Anyway, soka ni mchezo wa maajabu pia.

Tusubiri Madagascar Vs Benin.
 
Hata ukituambia nini sisi ni makolo tu
 
Machezaji yetu Hamna kitu kabisa.....yapoyapo tu huku tukifungwa. Mashenzi kabisa yamenikera sana.
 
Kwa uchezaji ule aiseee tz bado sana, chezaji linakaa nyuma ya adui halafu linaomba mpira. Hakuna nia ya kufunga wala hawakabi wanasubiri adui apoteze mpira wachukue. Hovyo kabisa aisee nimeona aibu sana leo.
Eti inapigwa kona mtu anakaa nyuma ya adui. Halafu wako kama hawali kidogo tu chini. Hovyo sana aisee hata kama wakienda huko wedi kapu watashangaa hawa wa wapi.
 
Kuna redio moja ilitahadhalisha kwamba wanasiasa waache kupeleka pressure kwa wachezaji ila hawakisikia kesho yake wakajifanya benchi la ufundi wakaweka viti na kuanza kupiga picha za kupost eti wanawapa hamasa. Yaliyotokea kila mtu anajua
 
waongo banah, hapo tunawaponda watu wa kwenye sekta ya mpira wa miguu na kuwaona kama mazuzu vile ukiangalia kila sekta kwe nchi yetu iko nyuma ukilinganisha na mataifa mengine unajiuliza hawa wanaotukana wenzao wa kwe mpira wao wamefanya revolution gan kwe industry zao hakuna anayeweza kukujibu, unakuta mchambuz yuko busy kumbeza mchezaji eti hajitumi apate nafasi ya kwenda kucheza nje unajiuliza ye alishajribu kutafuta nafasi ya kwenda kutangaza BBC no Yupo tu kwe kiredio local akipiga porojo, mwngne ni mwalimu kwe shule zetu zinazofelisha kil kukicha, mwngne ndo wanasiasa wetu ambao wanalalamikiwa na wanachi ila linapokuja swala la mpira kila mtu anaona ana mawazo sahihi na ni kazi rahisi tu kuyaweka kwe action matokeo yakaonekana
 
Mpira wa TZ nikama kumnenepesha ng'ombe siku ya mnada huku wateja wanamsubilia kumnunua
 
Mimi huwa nawashangaa sana baadhi ya watu hapa Duniani! Hivi Profesa wa Chuo Kikuu anaweza kumfundisha mtoto wa Chekechea kuhusu neuro surgery akamwelewa!
Unachukua wachezaji waliokimbia shule Manzese na Tandale unawapa kocha Mzungu awafundishe soccer waende kombe la dunia!
Mtaendelea kusubiri kwa muda mrefu sana Meli itie nanga Airport!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…