sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Na uzuri ni kwamba sayansi imekuwa kwa sasa, tunaweza kupima dna kujua kama watoto ni wetu lakini pia tunaweza kupima dna kutambua kama tumebeba genes zenye magonjwa ya kurithi kama vile ualbino, uziwi, ububu, ulemavu wa akili, n.k.
Mangonjwa yanayoweza kurithika hutokea pale ambapo watu wawili mwanaume na mwanamke wametokea katika familia zenye historia za ugonjwa au ulemavu unaofanana, wao wanaweza kujiona wazima lakini ukweli ni kwamba nao wamerirthishwa mbegu zinazoweza kutoa mtoto mwenye ugonjwa au ulemavu endapo mimba ikitungwa
Ili mtoto aweze kupatwa hali hizo za kurithishwa inabidi wazazi wote wawili wawe na gene ya hali husika, Yani mzazi moja pekee kuwa na gene ya hali husika haitoshi mtoto kuzaliwa na ugonjwa au ulemavu wa kurithi, na haimaanishi kwamba wazazi wote wakiwa na hizo genes za magonjwa ya kurithisha basi ni lazima mtoto atazaliwa na ugonjwa ama ulemavu, La Hasha!!! bado kuna asilimia kubwa sana ya kuzaa mtoto mwenye hali ya kawaida kabisa lakini watoto watabeba genes ambazo hapo baadae wakikutana na wenzao wenye genes zinazofanan basi watazaa mtoto mwenye ugonjwa/ ulemavu ama nae watamrithisha hizo genes.
Mfano kwa wazazi wa Manara ni kwamba wazazi wote walikuwa na hizi genes za ualbino na ndio maana kuna wanafamilia wengine wamezaliwa kawaida lakini Manara akarithishwa kwa kuzaliwa nao kabisa, Hivyo ingawa wazazi wote wa Manara wana ngozi za kawaida lakini wote walikuwa na genes za ualbino, hivyo usijione una ngozi ya kawaida ukadhani huwezi kupata mtoto albino. Kwa sasa Manara itakuwa kabla hajatunga mimba ni Lazima athibitisha mwanamke hana vinasaba vilivyorithishwa ualbino katika ukoo wake.