Tuache masihara, idara ya FBI ya Marekani wako Sayari nyingine kwenye mambo ya uchunguzi wa makosa ya jinai

Tuache masihara, idara ya FBI ya Marekani wako Sayari nyingine kwenye mambo ya uchunguzi wa makosa ya jinai

Hapa kwetu kesi moja ya Billionea Msuya Watuhumiwa mmoja wao Jina limenitoka alifanyiwa mateso yalompelekea hadi kumpa mke wake Talaka akiwa wakati wa upelelezi maana asingeweza kuwa mwanaume tena.

Na baadae ushahidi ukaonesha yeye hakuwa na Hatia na kuachiwa.
Yapo mambo Yanafanyiwa umakini hapa kwetu ila Sehemu kubwa Ni kutumia Nguvu si akili
Mrediii
 
Bongo TISS inafanikiwa kukusanya intelligence kwasababu wabongo ni wambea isingekuwa hivyo wangekuwa na wakati mgumu
 
Kuna kipindi nilisoma mtazamo wa mwenajukwaa huku anaitwa Nyani Ngabu kuhusu kesi ya mwanamuziki Robert Kelly ya unyanyasaji wa kingono, jamaa akasema FBI wakikushitaki uwezekano wa wewe kuchomoka ni chini ya 10% sikuamini saana. Akasema uwezekano wa R. Kelly kuchomoka ni mdogo sana sikutilia maanani sana.

Sasa kwa mwezi mzima huu nimekua nikiangalia documentaries za FBI files, kipindi cha matukio ya kihalifu yaliyochunguzwa na FBI na wahalifu kukamatwa, hakika nimeamini wale jamaa wako mbali sana, wako Sayari nyingine kabisa ya uchunguzi.

FBI wanaweza kukuchunguza kwa miaka 17 na mwisho watakukamata tu, ni nafasi ndogo saana watu kunusurika kutiwa nguvuni wakichunguzwa na FBI, wale jamaa wana matukio ya hadi ya miaka ya 30 na jinsi watuhumiwa walivyokamatwa kwa kweli wale jamaa hawafai.

Yup!

Feds conviction rate yake iko kwenye asilimia za juu za 90 huko. 95%-98%.

Huwa hawafungulii mashitaka ili mradi tu.

Wakikufungulia mashitaka basi ujue wana ushahidi ambao hata wewe mwenyewe mtuhumiwa huwezi kuukana.

Na ndo maana kesi zao nyingi huwa hata hazifiki kwenye hatua ya trial.
 
Kwanza kuchunguza tu kesi zaidi ya miezi sita huo ni udhaifu wa mbinu, na upigaji wa kijinga.

Hapa ndipo huwa naona udhaifu wa Mwanadamu.
 
Yup!

Feds conviction rate yake iko kwenye asilimia za juu za 90 huko. 95%-98%.

Huwa hawafungulii mashitaka ili mradi tu.

Wakikufungulia mashitaka basi ujue wana ushahidi ambao hata wewe mwenyewe mtuhumiwa huwezi kuukana.

Na ndo maana kesi zao nyingi huwa hata hazifiki kwenye hatua ya trial.
Mkuu nakubaliana na wewe 100%, FBI hawana mchezo. Jana nilikua naangalia hii ya episode, jamaa pamoja na kua alificha ushahidi karibu 100% ya kuhusika kwenye utekaji na uuaji lakini bado feds walimtia kifungoni.


Kuna ile moja ya DC gangs walivyomkamata Kobi Lawman hapa Tanzania mwaka 1994 baada ya upelelezi wa zaidi ya mwaka mmoja.

Nakubaliana na wewe kabisa mkuu.
 
Intelligence service ya Tanzania iko serious kwa viongozi wakubwa wa nchi ( Na vyama vyao), si kwa ajili ya taifa.
 
Back
Top Bottom