Tuache Siasa, Riba ya Mabenki ya biashara kukopesha Raia ni suala la Vihatarishi na sio maamuzi ya Serikali

Asante sana Mkuu 🤣 🤣 🤣 -Nimekuelewa
 
Ukisoma point No 1 na No 2 ya mleta UZI ndio utapata jibu la swali ulilouliza mkuu.
 
Mkuu usiongelee porojo-Be specific kwendana na policy requirements manake naona unazunguka zunguka tu,Hapa tunaongelea legal issues.
Mkuu hiyo sio mara ya kwanza kutokea au Serikali kufanya hivyo, Sera nyingi sana serikali imezifanya, Hiyo sera sio mara ya kwanza

TIB zamani mbona hayo yalifanyika na vigezo kibao mwisho wa siku Bank ikagawanywa, Biashara sio sera, Biashara ni kazi kazi na kuangalia faida basi

Unakumbuka mabilioni ya kikwete wakati anaingia madarakani yalipelekwa NMB Bank wakopeshe watu

NMB ilizipokea hizo billions za kikwete na kukopesha watu kama njugu kama serikali ilivyotaka,

Mwisho wa siku unafahamu Kilichotokea kwenye hizo pesa za bure za serikali kwenda NMB

Hizo pesa sio sustainable kwa Bank
Bank inatakiwa iwe na Customer Strong Deposit na sio hizo temporarily Injections za BOT

BoT kuna muda inasaidia Mabenki sana lakini wakiona wanawapa msaada bado wanashindwa ku mobilize Customer deposit wanaamua kufunga Bank husika

Achana na Siasa, Hizo pesa zinaweza pelekwa huko lakini hazitazaa matunda yeyote

Je Bank ya wakulima kwanini wanapambana si wana mtaji wa serikali na Serikali ina inject pesa huko, Hapa Bank lazima ijipange kutengeneza Strong Deposit Base na Strong Credit rating ya kutoa mikopo

Lini hizo policy zilifanya kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kingine, hii relif hii ilitolewa kwenye mikopo ya kilimo hasa. Kama rate ya kukopesha kwenye kilimo ni ndogo sana relief ya BOT huipati.
 
Wachumi wanatuambia kazi mojawapo ya bot ni kusimamia kiwango cha Riba kisiyumbe au kutetereka na kiwe kidogo kadri inavyowezekana.
Na kwa namna hio inakuza kasi ya ukuaji wa uchumi
 
Ujumbe uliotolewa na B.O.T ndio huu ulioandika hapa,pia umeskip kipengele kimoja muhimu sana kulingana na maelezo ya B.O.T hizo bank ambazo wataingia makubaliana inatakiwa mikopo itolewe kwenye shughuli za kilimo na sio vinginevyo
 
Ujumbe uliotolewa na B.O.T ndio huu ulioandika hapa,pia umeskip kipengele kimoja muhimu sana kulingana na maelezo ya B.O.T hizo bank ambazo wataingia makubaliana inatakiwa mikopo itolewe kwenye shughuli za kilimo na sio vinginevyo
Siyo kilimo pekee Mkuu, ingawa kilimo ni one of the priority sectors
 
Siyo kilimo pekee Mkuu, ingawa kilimo ni one of the priority sectors
"Kuanzishwa kwa mfuko maalum wa kukopesha mabenki na taasisi za fedha ili ziweze kukopesha sekta binafsi. Benki Kuu imeanzisha mfuko maalum wenye thamani ya shilingi trilioni moja ambao utatumika kukopesha mabenki na taasisi za fedha kwa riba ya asilimia 3, ili taasisi hizo ziweze kukopesha sekta binafsi. Benki au taasisi ya fedha itakayofaidika na mfuko huu itatakiwa kukopesha sekta binafsi kwa riba isiyozidi asilimia 10 kwa mwaka. Hatua hii itaongeza ukwasi na kupunguza riba za mikopo kwa sekta binafsi"
 
Kwa maana hyo ni hiari kuchukua huo mkopo, kwa hyo ukichukua vigezo na masharti kuzingatiwa na benki zisipochukua Ina maana hawalazomishwi kufuata hyo masharti.
 
Mkuu tuseme wewe ndio unakopesha una kamtaji kako..., unadhani kwa risky involved kwa watu ku-default Bongo ungeweza kufanya hizo Biashara kwa riba ndogo ukizingatia majority wanaweza wasilipe ?

Kumbuka hii ni Biashara na kutokana na Risky inabidi rates ziwe accordingly ama sivyo na wewe unaweza kujiunga na hao wakopaji soon or later kwa kufunga biashara yako na kutafuta mkopo...

Ingekuwa watu wengi ni Credit Worthy Benki zenyewe zingepanga foleni kubembeleza watu na kushusha riba to the minimum
 
una akili sana aise
 
Mpaka sasa Mimi nawafahamu waliokopa kwa 9% na 10%.kwa 6% bado sina data kwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Inachangiwa na nini riba kupunguziwa mkopaji? Je wale wanakopa nje ya nchi kwa USD, awapati athari au shida yoyote kutokana na shilling yetu kuwa WEAK dhidi ya DOLLAR?
 
Vipi kwa wafanyakazi wa serikali ambao wanakopea mishahara , na wenyewe wana risk ? Tz banks are just too greedy, wanataka over profit, hii sawa, serikali ilinde watu wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…