Tuache Siasa, Riba ya Mabenki ya biashara kukopesha Raia ni suala la Vihatarishi na sio maamuzi ya Serikali

Tuache Siasa, Riba ya Mabenki ya biashara kukopesha Raia ni suala la Vihatarishi na sio maamuzi ya Serikali

Nakubaliana na wewe. Mimi siyo mchumi lakini uzoefu wangu wa Marekani ni kuwa wakopeshaji wanatafuta watu wa kukopesha. Mabenki huwatumia watu barua kuwabembeleza wakope tena kwa riba ya chini kabisa.
Hapa Tanzania huwezi kufanya hivyo kuna mikopo mingi hazikopesheki tena
 
Ndo maana nikakwambia huna uelewa na taasisi za kifedha Tanzania,Unaongelea masuala ya shule na hisia zako binafsi.Be specific kwenye hoja zako pia,manake ukiulizwa huku unarukia kule-consistency ni muhimu sana kwenye arguments.
Mpaka Leo kuna Bank inakukopesha kwa asilimia chini ya 10%

Soko ni huria hili
 
Uzi mzuri, tusichanganye siasa, TZ benki bado ni nyonyaji kwa wateja wake
 
Kama ni hivyo kwa Nini wafanyakazi wawe na riba Sawa na hao unoita kapuku ili hali urejeshaji wao wa mkopo ni wa uhakika pia?
 
Kwa maana hiyo mtu mwenye biashara ya uhakika Kuna benk inaweza mkopesha kwa riba ya let's say 6%?
Wakati watu wengi wakienda benk kuomba kukopa wapo wafanyabiashara wanaofuatwa na bank kuwaomba wakakope kwao. Fikiria kuhusu riba za hiyo situation mbili
 
Benki zinajiendesha kwa taabu sana kutokana na ghalama kubwa za mitaji (fixed deposits). BOT wameweza toa hiyo rate kwa kuwa wana uhakika pesa yao by any means inarudi. Ukishindwa rudisha wanatoa kwenye minimum reserve yako iliyoko BOT, ambayo ipo kisheria na ikitolewa hiyo au kupunguzwa unakuwa hunasifa tena ya kuendesha benki wanakukalia kooni. Ukishindwa either benki itafungwa kwa kukosa sifa. Benki zinakopesha high risk projects ambazo nyingi hazirudishi pesa kwa wakati ambako kisheria benki huifuta mikopo michafu Vs their profits na hatimae kupata hasara. Rate za single digit na nk haliwezi endeshwa kisisa. Huu ni mtazamo wangu na si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom