Sabi Sanda
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 409
- 31
Wakuu,
Natumaini wengi wetu tumepata taarifa kuhusu matokeo ya darasa la Saba. Inatia aibu na kusikitisha sana kuona kuwa Hisabati ndiyo somo linaloongoza kwa wanafunzi kufeli. Zaidi ya asilimia 79 wamefeli. Ukienda ngazi ya sekondari hali haina tofauti kwani wastani wa wanafunzi wanaopata "F" katika Hisabati ni zaidi ya asilimia 75.
Nafikiri ni muhimu sana tukakubali udhaifu wetu na kufanya kile tunachopaswa kufanya kama taifa. Tuwekeze ipasavyo katika Hisabati na sayansi kama taifa. Tembeleeni vyuo vyetu vya ualimu muone hali ilivyo. Hivi kweli tuko makini kweli na ubora wa elimu katika nchi yetu????
Kuhusu somo la Kingereza takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 64.6 wamefeli. Moja ya njia inayoweza kutusaidia ni kufundisha Watanzania kwa angalau saa 2 kila siku kupitia Televisheni la Redio (hasa TBC). Tukiwekeza angalau shilingi bilioni 20 kila mwaka pale TBC kwa ajili ya kutoa elimu kwa taifa kwa kushirikiana na vyuo vyetu mbalimbali, baada ya miaka 10 tutakuwa taifa tofauti.