Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 9,397
- 12,415
Mtu wa Mungu, kumpokea Yesu hakuangalii dini ya mtu, ni moyo wako tu. Neno la Mungu linasema kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Anaye mpokea Yesu anapata uzima wa moyo, uzima wa akili, uzima wa ulimi hadi afya. Yesu anakupa amani ya kweli anakupa kuchukuliana. Heri yule awezaye kumwona mwenzake kwamba ni mjinga maana amefunuliwa hayo kwasababu ana hekima. Kwa hiyo asinge kuwa na haja ya kuanza kutukana zaidi ya kumwonea huruma kwasababu ya ujinga wake. Kwa maana Muhubiri 7:9 inaandika hivi "Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu."
Je wewe hupendi kujifunza hayo maneno mazuri baada ya kumpokea Yesu.
Mithali 4:23 inaandika Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. Moyo ndio chanzo cha mawazo yetu, maneno yetu, matamshi yetu, matendo yetu, na maisha yetu yote, hivyo tunapaswa kuulinda dhidi ya mambo mabaya. Yote haya Yesu anakufundisha bure kabisa ili uwe mzima.
Mithali 23:7 Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Yaani Unavyomwona mtu ndani ya moyo wake (mtazamo wake, imani yake, tabia yake ya ndani) ndivyo atakavyodhihirika katika maisha.
Lengo la Yesu kuja hapa duniani ilikua ni kutufundisha jinsi ya kuishi kwa amani, maisha ya haki, kuwa wavumilivu, kujishusha, kuchukuliana, kuwa wastahimilivu na kupendana. Kosa la Yesu liko wapi hapo kukufundisha mambo ya upendo, au kukufundisha kuchukuliana?.
Yesu anawapenda wote. Watu wana mizigo hawataki kuitua, mtu amebeba mawazo mabaya moyoni Yesu anasema katika Mathayo 11:28-30 "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifunzeni kwangu, kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."
YESU NI MFALME WA AMANI
YESU NI NJIA
YESU NI UZIMA
Daudi anazungumza katika Zaburi 119:11-12 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Ee BWANA, umehimidiwa, Unifundishe amri zako.
Ni Yesu pekee awezaye kuungoza moyo wako moyo ni mdanganyifu sana: Yeremia 17:9 "Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kuambukiza; nani awezaye kuujua?"
Siku zote moyo huwaza mambo mabaya tu ukishindwa kuucontrol utapata haya matokeo: Marko 15: 18-20
Lakini yanayotoka kinywani hutoka moyoni, nayo ndiyo yamtiacho mtu unajisi. Maana katika moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushuhuda wa uongo, na matukano. Hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi;
Ni nani sasa awezaye kuucontrol moyo kama mwanadamu anashindwa ni Yesu pekee.
Zaburi 32:8
"Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama."
Isaia 48:17
"Bwana, Mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye yakufaa, nikikuongoza kwa njia ambayo unapasa kuifuata."
Mithali 3:5-6
"Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako."