Naomba niulize nikimwomba Mungu kwa jina lake, inakuaje bila Yesu?
Maake hata Yesu alitufundisha kusali akisema
Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni,
utupe Leo riziki yetu,
Au Kuna sehemu Yesu kasema tuombe kwa jina lake ? Achana na kina Paulo au Petro Kuna sehemu Yesu kasema ombeni kwa jina langu ?
Yohana 14:13-14
Nanyi mtakayoyaomba kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Ikiwa mtaomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.
Yohana 16:23-24
Na siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mtakayoyaomba Baba kwa jina langu, atawapa. Hata sasa hamjaomba neno lo lote kwa jina langu; ombeni nanyi mtapokea, ili furaha yenu itimizwe.
Yohana 15:16
Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi, nami nimewaweka mwende mkazaae matunda, na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mtakalomwomba Baba kwa jina langu awapeni.
Marko 16:17
Na ishara hizi zitafuatana na wale waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya
Luka 10:17
Wale sabini wakarudi kwa furaha wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.
Matendo 16:18
Alifanya hivi siku nyingi. Lakini Paulo akakasirika, akageuka, akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo mtoke katika huyo. Akatoka saa ile ile.
Matendo 2:38
Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Mathayo 28:18-20
Yesu akakaribia, akasema nao, akisema, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Marko 16:15-18
Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini atahukumiwa.
Na ishara hizi zitafuatana na wale waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa; watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.