Tuache vita, Dunia itulie

Tuache vita, Dunia itulie

rr4

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
3,797
Reaction score
5,510
Hivi hatuezi kuacha kurushiana Risasi?
Tukae chini tushikamane tuimbe nyimbo za amani.

Wenye njaa wasaidiwe, wasio na mavazi wavishwe, ambao hawana makazi wapate Makazi?

Kwani ni lazima vita virindime kila siku.?
Wenye madai ya ardhi wapewe nchi zao.

Kama Zanzibar anapiga kelele aachiliwe basi aachwe huru.

Na Kila mtu atawale nchi yake, asiende kuwa kiongozi kwenye nchi ya mwenzake.

Hii JD of 2025 yaani (JAMII FORUM DECLARATION OF 2025) ulipaswa uisemee kwenye vikao vya security council. Huku hutasaidika na hawa wachangiaji wa Ngudulugulu,Sumve,Nyangwale na Kiabakari.
 
Vita vilikuwepo tokea mwanzo wa dunia.
Soma biblia yako na quran yako utaviona.
1. Makabila hapo zamani yalipigana vita
2. Yule muislamu aliyeuteka Mji wa Maka na kupiga adhana ya kwanza alipigana vita
3. Joshua kuuteka mji wa ahadi, alipigana vita.

Tena vitabu vya dini ndio vina VITA KIBAOOO.
Tena vita nyengine zilibalikiwa...!!!

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
VITA NI BIASHARA.
UNAPOTOKA NYUMBANI KWAKO KWENDA KUTAFUTA RIZKI NAYO NI VITA
 
Inasikitisha sana...

Cc: Mahondaw
Sana.
Sudani hakufai
Somalia hakufai
Congo Drc hakufai
Africa ya kati hakufai
Chad Kwa moto
Msumbiji kama hivyo
Libya kunanuka
Tanzania kutekwa ni sekunde
Rwanda ni suala la muda TU

Na , duniani ndio kama tunavyosikia.

Mi nadhani nguvu kubwa itumike kuangalia maendeleo ya watu sio vita na kununua silaha.
 
"Ili mmoja ashibe lazima mwengine aumie."

Hii ndo system ambayo dunia inarun.
Ukiangalia nchi zote zilizoshiba yaani zilizoendelea zote zilipitia vita at some point kwenye maendeleo yake.

China ilipigana na Japan, South Korea, Uingereza na mataifa mengine mengi mpaka tunaiona China ya leo.

Vivyo hivyo Marekani imeshapigana na Mexico, Vietnam na Uingereza na mataifa mengine kama Urusi hadi ikawa Superpower.

Kwahiyo namna pekee ya kuzuia vita zisitokee ni kufanya dunia iwe nchi moja.
 
Ili VITA ziishe basi lazima MIGODI yote isifanye kazi ..kuanzia metal, copper MPAka Vito yaani natural resources zote zihifadhiwe kwa muda watu wasichimbe
 
  • Thanks
Reactions: rr4
"Ili mmoja ashibe lazima mwengine aumie."

Hii ndo system ambayo dunia inarun.
Ukiangalia nchi zote zilizoshiba yaani zilizoendelea zote zilipitia vita at some point kwenye maendeleo yake.

China ilipigana na Japan, South Korea, Uingereza na mataifa mengine mengi mpaka tunaiona China ya leo.

Vivyo hivyo Marekani imeshapigana na Mexico, Vietnam na Uingereza na mataifa mengine kama Urusi hadi ikawa Superpower.

Kwahiyo namna pekee ya kuzuia vita zisitokee ni kufanya dunia iwe nchi moja.
Ambayo tunaambiwa ndio New world Order.

Kama itakuwa for the benefit of all humanity ije tu.
 
Back
Top Bottom