Tuambiane ukweli Je Kuna siri gani kwenye kuimba/Mziki?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,463
Reaction score
27,556
Nina amini kuna siri kubwa sana kwenye kuimba haijarishi unaimba katika lengo gani.
Tukianza na kwenye tamaduni zetu za kijadi karibia kila kusanyiko nyimbo huhusika yaani burudani.

Angalia kwenye Dini iwe ukristo au uislamu nyimbo zinahusika pakubwa sana kwenye uislamu utakuna na kaswida
kwenye ukristo kuna kwaya na wameboresha hadi lege na sebene utaipata makanisani....

Kitabu cha kutoka kimeandika wazi kuwa wana wa Israel waliimba wimbo punde tu walipoivuka bahari ya shamu.
pia tunasoma kwenye kitabu cha matendo kuwa paulo na sila waliimba mle gerezani hadi milango ya gereza lile ikafunguka.

Hata shetani (lusifa) anasemwa alikuwa ni mwimbaji mzuri sana mwenye sauti zote na zilikuwa zinatoka kwa pamoja na kwa mpangilio ulio tukuka sana.

Kwenye mambo yote burudani bila mziki hakuna sherehe hapo tangu nizaliwe hadi leo sijawahi kuta sherehe bila kuimba iwe ni ya jadi ama kisasa bado mziki uwepo basi hata ngoma utasikia.

Ukienda kwa waganga wa kienyeji kua muda mizimu huwa inaimbiwa nyimbo ili ifurahi na kumfanyia wepesi mganga huyo katika kazi zake.

Misibani napo kuna nyimbo zake za kuombeleza /masikitiko bila shaka peter msechu kajizolea umaarufu kupitia nyimbo zake za maombelezo hasa za watu maarufu wa nchi hii.

Kwenye shughuli za kisiasa mtakuwa mashahuda nyote wasanii wetu husombwa kwa gharama kubwa ili tu wakanogeshe makongamano/mikutano hiyo.

Huku wasukuma kila wanapofanya kazi zao za kilimo lazima utasikia nyimbo na nyimbo na hata wafanyakazi wa Tanesco utasikia wakiimba nyimbo zao za matusi ya nguoni nk lakini zote ni nyimbo

Inasemakana hata huko kwenye ulimwengu wa wenzetu wachawi nyimbo ni kipaumbele sana na hayo yanajiri pale unapoangalia movie za kichawi japo wanaigiza hivyo chukulia kuwa kuna nyimbo pia kule...

Marehemu Remy ongala aliwahi kuimba kuhusu umuhimu wa muziki.. "Mziki asili yake ..."

Mziki una siri gani wakuu?
 
Muziki ni burudani ya asili inaburudisha,kuelimisha,kufundisha, na kufurahisha. Naweza kusema sauti zimekuwepo tangu enzi na enzi, muziki ni sauti hakuna sauti hakuna muziki.

Muziki ni kama sehemu ya kuappreciate uwezo wa viumbe hai kusikia sauti.
Kama wewe ni kiumbe hai lazima uufurahie muziki haijalishi ni muziki gani utakaoufurahia, ila lazima kuna aina fulani ya muziki utaipenda.
 
Ukitaka kujua siri ya mziki Kula chuma hiki hapa
 
Attachments

  • MERCY_JOSEPH_-_LER_NORIENY__OFFICIAL_HD_VIDEO__SMS__Skiza_6987754__to__811_(360p).mp4
    12.4 MB
Ya kwamba mizimu inaimbiwa ili ifurahi...🤣🤣🤣
Mkuu hapa duniani kuna mambo sana mengi tu tusiyo yajua hata nusu yake.
Mara ya kwanza kuona watu wanaimbia mizimu ni kwa mganga nilienda kumsalimia mgonjwa (mama mdogo) watu waliimba na kucheza na kucheza chinja mbuzi mizimu imenuna tu hadi badae sasa ikakubali na kumachia mgonjwa yule...sitasahau
 
Muziki ni burudani ya asili inaburudisha,kuelimisha,kufundisha, na kufurahisha. Naweza kusema sauti zimekuwepo tangu enzi na enzi, muziki ni sauti hakuna sauti hakuna muziki.

Muziki ni kama sehemu ya kuappreciate uwezo wa viumbe hai kusikia sauti.
Kama wewe ni kiumbe hai lazima uufurahie muziki haijalishi ni muziki gani utakaoufurahia, ila lazima kuna aina fulani ya muziki utaipenda.
Hakika
 
Nina amini kuna siri kubwa sana kwenye kuimba haijarishi unaimba katika lengo gani.
Tukianza na kwenye tamaduni zetu za kijadi karibia kila kusanyiko nyimbo huhusika yaani burudani.

Angalia kwenye Dini iwe ukristo au uislamu nyimbo zinahusika pakubwa sana kwenye uislamu utakuna na kaswida
kwenye ukristo kuna kwaya na wameboresha hadi lege na sebene utaipata makanisani....

Kitabu cha kutoka kimeandika wazi kuwa wana wa Israel waliimba wimbo punde tu walipoivuka bahari ya shamu.
pia tunasoma kwenye kitabu cha matendo kuwa paulo na sila waliimba mle gerezani hadi milango ya gereza lile ikafunguka.

Hata shetani (lusifa) anasemwa alikuwa ni mwimbaji mzuri sana mwenye sauti zote na zilikuwa zinatoka kwa pamoja na kwa mpangilio ulio tukuka sana.

Kwenye mambo yote burudani bila mziki hakuna sherehe hapo tangu nizaliwe hadi leo sijawahi kuta sherehe bila kuimba iwe ni ya jadi ama kisasa bado mziki uwepo basi hata ngoma utasikia.

Ukienda kwa waganga wa kienyeji kua muda mizimu huwa inaimbiwa nyimbo ili ifurahi na kumfanyia wepesi mganga huyo katika kazi zake.

Misibani napo kuna nyimbo zake za kuombeleza /masikitiko bila shaka peter msechu kajizolea umaarufu kupitia nyimbo zake za maombelezo hasa za watu maarufu wa nchi hii.

Kwenye shughuli za kisiasa mtakuwa mashahuda nyote wasanii wetu husombwa kwa gharama kubwa ili tu wakanogeshe makongamano/mikutano hiyo.

Huku wasukuma kila wanapofanya kazi zao za kilimo lazima utasikia nyimbo na nyimbo na hata wafanyakazi wa Tanesco utasikia wakiimba nyimbo zao za matusi ya nguoni nk lakini zote ni nyimbo

Inasemakana hata huko kwenye ulimwengu wa wenzetu wachawi nyimbo ni kipaumbele sana na hayo yanajiri pale unapoangalia movie za kichawi japo wanaigiza hivyo chukulia kuwa kuna nyimbo pia kule...

Marehemu Remy ongala aliwahi kuimba kuhusu umuhimu wa muziki.. "Mziki asili yake ..."

Mziki una siri gani wakuu?
Mtoto wa miez 2 ukimuimbia au akisikia muziki anatabasamu alaf anachezesha mikono na miguu.
Muziki hatari
 
Back
Top Bottom