storyteller
JF-Expert Member
- Nov 5, 2014
- 1,511
- 1,844
Utundu wa kwenda kuwazingua vichaa pale milembe ndogo, siku moja kidogo ututokee puani......
Tulikua tunavuka seng'enge tunaingia kwenye mabweni yao.... tunazingua wakianza kutukimbiza tunawachengesha..... kisha tunawapoteza maboya tunarudi kwenye seng'enge tunatoka..... kwa kweli sijui tulikuwa tunaona raha gani wakati ule......
Siku moja kumbe kuna mmoja mwenzetu aliyetutangulia akanaswa na seng'enge..... weeeeeeh!..... tuliparamiana..... kwa akili ya haraka sana nikapanda kwa juu badala ya kusubiri tundu......... wenzangu nao kuona vile na kwa vile wale vichaa wamekaribia.... wakaruka.... tukamuamuru mwenzetu avue kaptura(enzi zile hata chupi hatuvai)... hiyo ikawa pona yake.
Tangu siku ile kuna kichaa mmoja akawa habanduki kwenye lile tundu..... kumbe nao wakawa wanatoroka kupitia lile tundu letu hadi pale wahudumu walipogundua hilo tundu.