Tuambie kitu cha utundu sana ulichofanya utotoni na hutakisahau maisha yako yote

Tuambie kitu cha utundu sana ulichofanya utotoni na hutakisahau maisha yako yote

Nakumbuka walikua wanapiga wezi na kuwachoma.Walikuwa wawili watu wamekusanyika barabarani nami nkiwa mdogo.Kugeuka naona kuna Mzee alikuwa jirani yangu amevaa jacket refuu.Kuna shillingi noti za miambili miambili jumla mia nne.Basi nkazichomowa nkaondoka huku moyo unandunda nkazieka mwezi mzima chini ya jiwe la kusugulia miguu nlifunga katika karatasi ya plastic.
Yaani, mwizi anasulubiwa nawewe unaiba hapo hapo?
 
Darasa la sita tushamnusa sana makalio mwl mmoja hivi alafu rafiki yangu alikua mshenz anapiga na chafya kabisa. Kucheka ni mpaka Mwl atoe kichekesho ndo tunacheka hadi chini vipo vingi aiseh
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Darasa la sita tushamnusa sana makalio mwl mmoja hivi alafu rafiki yangu alikua mshenz anapiga na chafya kabisa. Kucheka ni mpaka Mwl atoe kichekesho ndo tunacheka hadi chini vipo vingi aiseh
Mafirauni kabisa
 
Mimi niliwahi kuiba mishale ya Uncle,, nikaona ni mikubwa sana siwezi kuitumia nikaamua kutoa ile chuma ya mbele niweke kwenye mshale wangu,, nakashindwa ikanibidi kung'oa kwa meno ebwanaeeh!! Nilichanwa mdomo, ilibaki kidogo nitoboke mdomo halafu,, mshale ulikuwa wa sumu ni bahati yangu sumu haikugusa damu,, ni dakika 3 tu ningekufa,, kurudi home nikavunga acha nivamie mapera,, asubuhi domo limevimba kama buti la mjeda,, mpaka leo sikusema nilifanyaje,, zaidi walihisi niliiba nyama nikachanwa na mfupa, ila ilibaki kuwa siri yangu leo ndo nimeitoa hapa[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] sitakaa nisahau utundu huo maana ungeniua
 
Itabidi nijitahidi kupanga yapi angalau yawe top 3, ilikuwa 😉 na shuleni kitabu nakibamiza kama kawa.
 
Kidato cha kwanza hapo,mwalimu wa History kaandika notes ubao mzima sema alikuwa na mwandiko wa hovyo,tumemaliza kuhesabu namba nikazama class nikaucheki mwandiko sikujua kama ni wa mwalimu nilijua ni wanafunzi tu walikuwa wanachezea ubao,nikaandika kwa maandishi makubwa kabisa WHICH KIND OF THIS RUBBISH nikasepa zangu maana halikuwa darasa langu,muda wa pindi ukafika na teacher akazama class kuelezea notes zake,ile anafika kuangalia ubaoni akakutana na hayo maneno,form I B walichezea kichapo havy na hakuna aliyeniona sijui wangemtaja nani sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku niliwahi sana shule kabla ya mtu yeyote nikaenda kuandika matusi ubaoni kwa herufi kubwa. Kilichofuata hapo ilikua ni dimbo class nzima siku tatu mfululizo tumtaje alieandika. Hatimae wakatajwa washkaj wengine ambao walikuaga watunduwatundu na wakaamriwa kuita wazazi wao halafu ikagongwa kengele wakachapwa tena mbele ya shule nzima halafu wanafunzi wote tukaamrishwa kuwazomea. Kwa jinsi nilivyokua mpole walimu waligoma kama ni mimi naweza kuandika yale matusi ubaoni maana kuna jamaa mmoja alinitaja kwamba aliniona asubuhi natokea darasani akasema huenda mi ndio niliandika.
Hahahaah dogo tena na ulivyo na vurugu za chinichini hao jamaa walipata taabu sana.
 
Back
Top Bottom