Tuambie sababu iliyokupelekea ukawa unatumia hiyo ID yako hapa JF

Tuambie sababu iliyokupelekea ukawa unatumia hiyo ID yako hapa JF

Fohadi

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2020
Posts
772
Reaction score
2,421
Binafsi naamini kila mmoja ana sababu yake iliyomfanya kujiita hilo jina anatumia hapa JF. Sio mbaya ukitufungulia password za jina lako. Kuna wengine IDs zao zimebeba historia au tukio fulani nyuma yake. Kuna wengine IDs zao pengine ni majina ya watu au vitu walivyowahi au wanavyoendelea kuvihusudu. Jaribu kutupa maana na sababu ya kutumia hiyo ID.

Mimi nilijiita FOHADI kwa sababu ni moja ya kanuni zangu za kila siku ambapo kila nikilikumbuka jina langu nakuwa nimejikumbusha kitu muhimu sana kwajili ya maisha yangu.

FOHADI ni abbreviation ya maneno Focus, Hardwork and Discpline.

Share nasisi kwanini ulichagua hiyo ID miongoni mwa majina mengine.​
 
Siku nafungua hii account nilikuwa kwa mwana afu pembeni akawa na wireless keyboard. Basi kama mnavyoujua keyboard ya computer ina button nyingi.
So nikajipa jina hilo la "Caps Lock" na dp nikapiga picha halisia ya hyo keyboard ila nikai crop hiyo picha ili button ya caps lock ionekane.
 
kuna Mkuu mmoja atapita hapa mda sio mrefu..anajiita cocastic ila mimi najua kwanini anajiita hivyo..najua hatatoboa hiyo siri ila ngoja niwaibie siri yake.

siku moja miaka mingi kidogo imepita mimi nayeye tukiwa wanafunzi kutoka shule mbili tofauti mkoani Dsm tulikutana sehemu kwa mdahalo maalumu wa wanafunzi. Wakati namalizia mchango wangu kwenye ule mdahalo, nilimalizia kwa maneno haya 'thank you so much organizers for the fantastic debate'.... Sasa ilipofika zamu ya huyu mkuu nae ikabidi apige chabo kidogo akasema 'I feel so lucky to participate in this cocastic debate'...Ukumbi mzima ulivunjika mbavu.

Basi ameona ndio iwe ID yake hiyo..​
 
Siku nafungua hii account nilikuwa kwa mwana afu pembeni akawa na wireless keyboard. Basi kama mnavyoujua keyboard ya computer ina button nyingi.
So nikajipa jina hilo la "Caps Lock" na dp nikapiga picha halisia ya hyo keyboard ila nikai crop hiyo picha ili button ya caps lock ionekane.
ulitisha sana kiongozi
 
Back
Top Bottom