Tuambie sababu iliyokupelekea ukawa unatumia hiyo ID yako hapa JF

Tuambie sababu iliyokupelekea ukawa unatumia hiyo ID yako hapa JF

Nilijikuta tuu naandika hili jina kutokana na msongo wa mawazo niliokuwa nao nakuwafikiria binadamu walivyo na roho za kisasi(kinyama) halafu wengi wao wao wanajifanya wameishika sana Dini kumbe ni wachawi wakubwa
 
Hili jina Chakorii nililipata kutoka kwenye movie ya kihindi inayoitwa Udaan kama sijakosea.

Main character aliitwa Chakor..ila mimi niliongeza ii mbele kwa kuwa watu wa kanda ya kaskazini hupenda kuongeza herufi kwa mbele.

mfano:
pita-pitaa
Vero-veroo
Rama-ramaa

Yani hivyo tu
Hahaaa nmekusoma sana!! Esta-Estaa
,John-Johniii
[emoji2][emoji2][emoji2]Kaskazin bhana
 
Shabiki,
Nilikuwa natembelea forum bila kuregister kwa miaka 2 ,
Kisha Nikavutiwa na mijadala,
Halafu kukawa na kamjuano ka watu wa MMU na Chitchat (Hii ni miaka ya 2012), wale watu wanacoment kwa kujuana, ukizamia post na yako wataipita kama hawaioni. Mpaka uwe maarufu. Ndio chanzo ya kuanzishwa makapuku forum baadae.

Nikaona sio lazima wote tucheze. Wengine tunaweza baki kuwa mashabiki tu. (Hata guru la falsafa Afande sele alishalisema hivyo kwenye mtazamo.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nilijikuta tuu naandika hili jina kutokana na msongo wa mawazo niliokuwa nao nakuwafikiria binadamu walivyo na roho za kisasi(kinyama) halafu wengi wao wao wanajifanya wameishika sana Dini kumbe ni wachawi wakubwa
Huu ni ukweli mchungu
 
At first naingia humu niliingia na jina langu halisi ilikua year 2014.
Sikua wa vile sana jukwani.
Ila kunakitu nilinotice kuwa member wengi walikua na majina ya kubuni.
Sasa nikaona nami ni buni la kwangu, ID haina maana yoyote, zaidi yakuwa tu muda uwo ambao niliamuaa kutengeneza ID nyengine ulikua ni muda wa Dochi Vele sa 7 mchana.
 
Ilalalaaaa Ilalaaaaa La Familiaaaaa Mikono Mfululu yaani papapapapapaaa wamekaaaaaaa!!

 
Binafsi naamini kila mmoja ana sababu yake iliyomfanya kujiita hilo jina anatumia hapa JF. Sio mbaya ukitufungulia password za jina lako. Kuna wengine IDs zao zimebeba historia au tukio fulani nyuma yake. Kuna wengine IDs zao pengine ni majina ya watu au vitu walivyowahi au wanavyoendelea kuvihusudu. Jaribu kutupa maana na sababu ya kutumia hiyo ID.

Mimi nilijiita FOHADI kwa sababu ni moja ya kanuni zangu za kila siku ambapo kila nikilikumbuka jina langu nakuwa nimejikumbusha kitu muhimu sana kwajili ya maisha yangu.

FOHADI ni abbreviation ya maneno Focus, Hardwork and Discpline.

Share nasisi kwanini ulichagua hiyo ID miongoni mwa majina mengine.​
Santos jina langu 06 ni nafasi yangu uwanjani
 
kuna Mkuu mmoja atapita hapa mda sio mrefu..anajiita cocastic ila mimi najua kwanini anajiita hivyo..najua hatatoboa hiyo siri ila ngoja niwaibie siri yake.

siku moja miaka mingi kidogo imepita mimi nayeye tukiwa wanafunzi kutoka shule mbili tofauti mkoani Dsm tulikutana sehemu kwa mdahalo maalumu wa wanafunzi. Wakati namalizia mchango wangu kwenye ule mdahalo, nilimalizia kwa maneno haya 'thank you so much organizers for the fantastic debate'.... Sasa ilipofika zamu ya huyu mkuu nae ikabidi apige chabo kidogo akasema 'I feel so lucky to participate in this cocastic debate'...Ukumbi mzima ulivunjika mbavu.

Basi ameona ndio iwe ID yake hiyo..​
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Niliandika majina mengiiiii
Naona yote wameshawahi

Niliandika hadi neno Antarctica nakuta watu wamewahi hilo jina


Nikafikiriaaa weee
Anyway enzi hizo lil pump ndo alitoaga huo utopolo wa gucci gang
Kwa hasira nikaandika gucci gang alafu nikasend nikijua itarudi kwamba limeshatumika....
Ndo mpaka leo mimi naitwa gucci gang
Sio kwamba nalipenda jina
Ila ni bahati mbaya tu
Na frastueshen zangu[emoji23][emoji23]
[emoji16]
 
Hili jina Chakorii nililipata kutoka kwenye movie ya kihindi inayoitwa Udaan kama sijakosea.

Main character aliitwa Chakor..ila mimi niliongeza ii mbele kwa kuwa watu wa kanda ya kaskazini hupenda kuongeza herufi kwa mbele.

mfano:
pita-pitaa
Vero-veroo
Rama-ramaa

Yani hivyo tu
Kama vile mimi naitwa Chalii
 
Back
Top Bottom