Tuambie timu yako ilitolewa hatua gani CAFCL?

Tuambie timu yako ilitolewa hatua gani CAFCL?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Kila mmoja anaisifia Mamelod kuwa ni timu tishio msimu huu lakini hawasemi Mamelod amefikaje hapo

Kabla ya kufuzu Nusu fainali msimu huu Mamelod amecheza Robo Fainali 4 mfululizo na kutolewa zote

Raja Casablanca ndani ya misimu mitatu mfululizo wanatolewa hatua ya robo fainali

Mpaka sasa Simba tumecheza Robo Fainali 3 za ligi ya mabingwa halafu anatokea mtu anakuambia Simba haistahili sifa maana Robo Fainali wameshacheza sana

Hatuvimbi kichwa kuishia Robo Fainali lakini tunajipongeza kwa kuwa na uthabiti (Consistency) hatujapiga hatua kubwa kwenda mbele lakin hatujarudi nyuma hata hatua moja

Tangu mwaka 2018 ni timu tano tuu zimekua na uhakika kucheza Robo Fainali mfululizo ikiwemo Simba nyingine zimeingia na kutoka

Tunapokea ukosoaji kuwa sasa tunatakiwa kutoka hapa na kusonga mbele zaidi Lakini tunasubiri kupiga hatua mbele ni lazima tujivunie hiki tulichopata

𝐌𝐩𝐢𝐫𝐚 𝐧𝐢 𝐦𝐜𝐡𝐚𝐤𝐚𝐭𝐨 𝐧𝐚 𝐥𝐚𝐳𝐢𝐦𝐚 𝐭𝐮𝐡𝐞𝐬𝐡𝐢𝐦𝐮 𝐦𝐜𝐡𝐚𝐤𝐚𝐭𝐨

My Take
Katika Ligi ya Mabingwa, timu yangu ilitolewa hatua ya robo fainali yaani 8 bora. Tuambie timu lako ilitolewa hatua gani katika Ligi ya Mabingwa
 
IMG_20230429_200918.jpg
hongera kwa kunyanyua ndoo

IMG_20230429_110601.jpg
 
Huu sasa utani wa ngumi,
UTOPOLO FC hawawezi kujibu hili.

Mashabiki wa utopolo wakiwa na mwiko nyuma akili zinawaruka.
 
Timu yetu mbumbumbu fc Kila msimu wa mashindano tunaishia robo na mwekezaji anadai ameshatumia bilioni 55 Kwa miaka 4 mpaka Sasa na hatujapata mafanikio.

Wasiwasi tulionao ni Kwa mwekezaji kama ataweza kutoa pesa nyingine za uendeshaji watimu kwakua bilioni 55 alizoweka zimepotea na hakuna dalili za mafanikio.
 
Back
Top Bottom