Imagine...Aisee, na chuma yako ya wa-NAZI
Vile vile range rover eti ukiikimbiza hadi sped ya mwisho kwenye dush board eti kuna kioo ambayo kuna picha ya mtu anapita akiwa kajitwika jenezaImagine nikiwa mdogo nliambiwa ETI Range rover haziruhusiwi kupaki benki, kwa sababu eti zina speed kali kwa hiyo zikitumiwa na majambazi kupora, polisi hawawezi kuzifukuzia wakazipata.
Halafu pia eti, Range rover huwa hazipinduki, eti kwa sababu tairi zake huwa zinatanuka gari ikitaka kupindiuka au ikiwa inakata kona kali ikiwa speed.
Mlionilisha haya matango pori hamuendi mbinguni.