Tuambiwe ukweli: Stiglers Gorge inaweza kuwa maafa makubwa kwa taifa badala ya furaha

yalijengwa kwa 3 years?umesoma thread ukailewewa?Aswan yenyewe ilijengwa for 11 years ,The Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD) tangu 2011 inajengwa.
Nimezungumzia MUDA WA KUJENGA, ENVIROMENTAL ISSUES,ECONOMIC ISSUES.hiyo 3.6 ni gharama halisi kweli siyo 8.5 billion dollars?siyo mtu anaondoka madarakani ndipo tunaanza kusema laiti tungejua na selous ni issue nyeti sana mkuu hilo li selous ni kubwa kama nchi ya uswisi na ni 4/5 ya nchi ya Ireland na eneo kubwa ni maji na viumbe hai unaelewa utofauti na maeneo mengine unayotaja?
 
Majadiliano ndilo suruhisho la mambo mengi sema tu tunajitoa ufahamu. Nakumbuka wakati mwingine aliyetoa mawazo tofauti na 'walioyataka' aliitwa msaliti lakini ukweli kwamba 10% ya leo kwenye project tusipoangalia vizuri inakuja kutugharimu 1,000% na waliokula hii 10% watakuwa hawapo. Then utasikia slogans za 'waafrika tuna akili ndogo'!
 
cha msingi hapo kama kuna hidden cost sawa lakini teknolojia sina shaka na timefre waliyojingangia solution ilikuwepo kipindi cha nyerere sio ya Leo . tupo kwenye zama za digital kwa hiyo sitashangaa project kuisha chini ya muda
 
Prophets of doom
 
Yaani inasikitisha, eti watajenga usiku na mchana, kwani si kuna muda zege linatakiwa liachwe likomae lenyewe? Sasa hata nondo zitakapoungwa na kujengewa kabla hawaja jiridhisha ziko sawa si hatari kubwa? Kweli ccm wamezoea mchaka machaka hata kwenye mambo ya msingi Mungu baba tunusuru na janga la huu mradi.
 
Sasa huyu bwana asipomaliza nani atabaki analimalizia bwawa maana kila mtu na kipaombele chake
 

Bro, Cool down man, mambo sio mabaya kama unavtyotaka kutuaminisha, relax

Ingawa hata mimi naona 3 years imebana lakini kwa taarifa yako mambo yote hayo na EIA yalifanyika muda mrefu sana, enzi za Nyerere na mradi mzima ulikuwa kwenye mafail. Sawa kuna impact za muda kwenye climate change n.k lakini hawaanzi from scratch. Mimi niliwai kukusanya data za hydrology eneo hilo, niliona masalia ya aidha Norplan au NorConsult sina uhakika.
 
Mkuu mazingira tayari tushaanza kuyaharibu na hapo linapojengwa ndipo penye misitu mikubwa sana ya asili,na wanyama wanagongwa kila uchao na madereva wa kwenye mradi.
 
yaaps hale ilijengwa karbun 5 yrs na kukamilika 1995 kwa msaada wa sweeden, denmark na ukrain, lina SQM takriban 65 na urefu wa km 1.8 na kwa sasa wanazalisha MW68 na volt 11, ambapo husambazwa, tanga, dodoma, singida, arusha, morogoro, manyara na zenji yote, huku tanga ikipokea moha kwa moja kutoka hale hao wengne wakipokea kupitia gage ya taifa, sasa unaweza uka imagine MW68 tuu zinasambazwa kote huko, vip hizi MW2100 ukubwa wake utakuwaje? Na wao wenyewe wanasema changamoto kubwa ni pressure ya maji, ambayo huongezeka kudr kina kinavyozid, tunajua
P(in liquid)=density*height*gravity, sasa hale ni 1.8km vp hawa wa 8km na ushee? In 3yrs,
too many dramas in this country.
 
hata gesi ya Mtwara tuliambiwa ndiyo m40 wa kila kitu, leo hii mwenyekiti wa sasa wa chama chetu anasema eti wizi mtupu.
mwenyekiti mpya atakayembadili huyu wa sasa naye ataipiga chini Stiegler's Gorge kwa kudai ni "mradi wa kikolomije"!

poleni Watanzania.... ndiyo DNA ya chama chetu hiyo!
 
Hivi huwa kuna Nzagambajike pia?
 
Ishu ya namna hiyo kwani ni ngeni kabisa nchini Tz?

Kidatu na Mtera mbona hatujasikia zikipasuka na kuzagaza maji kama unavyohofia wewe?

Mikataba ya ujenzi inasemaje kuhusu uzembe utokanao na ujenzi hafifu nk nk?

Suala la ujenzi sijui kwanini shetani huwaga anakasirika sana?

Utakuta hata unapoamua kujenga nyumba binafsi lazima uwe msiri sana, vinginevyo ikifahamika mapema hiyo project yako, itapigwa vita hata na ndugu zako wa damu na mwisho wa siku kushindwa kutekeleza lengo ulilokusudia!

Ujenzi wowote ule, kabla ya kumalizika lazima huambatana na kuharibu mazingira ili kupata sura halisi ya unachokijenga.

Je kwa ushauri wako huu, ujenzi uahirishwe ama plan gani 'b' ifuatwe kuweza kupata umeme mwingi uliokusudiwa kukidhi mahitaji ya nchi?
 
Ni hivi..watu wameshajua jinsi ya kumpiga pesa huyu mkemia anayejifanya kila kitu abajua. Yan wao wanampa support tu ili wapate vitenda, mambo yakiharibika wanakaa kimya ila pesa wameshakula
 
Norplan ndio nini?
 
Status ya huu mradi ikoje ukizingatia na aliyeanzisha amelala milele(RIP KPM)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…