Tuambizane wimbo gani wa Mama uliwahi kukubamba?

Ile ya Yamoto Band ikichagizwa na sauti ya mawimbi ya mwimbaji wa taarabu ingawa si maarufu sana lakini tamu sana
 
Unajua wakati mama yangu yuko hai sikuwa naguswa sana na nyimbo zenye ujumbe wa mama lakini toka bi mkubwa afariki tarehe 20/04/2019 dah huo wimbo wa Christian Bella na Ommy Dimpoz kiukweli moyo uwa unaniuma sana na nakuwa natamani wakati huo unapoimbwa niwe na bi mkubwa wangu na mfano hai ni jumamosi tu iliyopita nilikuwa sehemu harusini ukapigwa huo wimbo kiukweli machozi yakawa yanataka kunitoka mbele ya watu nikanyanyuka na kwenda maliwatoni. Nakuombea mama yangu kwa ALLAH akusamehe makosa yako ya siri na ya dhahiri kwani yeye ni mwingi wa kusamehe na twamuomba pia alifanye kaburi lako ni miongoni mwa viwanja ktk bustani ya peponi!
 
Mwanzoni ilikuwa ni Dear Mama wa 2pac then wa Spice girls then wa Boys to men zilikuwa zinaniteka ila kiukweli kwa sasa wa Christian Bella ndio funga kazi
 
Yes rasta! One of the best from Sizzla! Luv u mama
 
Vijana wa zamani tunakumbuka wimbo
Mkali wa mama ulioimbwa na bendi ya
Muziki wa dansi, Tancut Almasi
Iliyokuwa na maskani yake mkoa Iringa,
Na mtindo wao kinyekisonzo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…