Tuamke, twendeni tukalime

Tuamke, twendeni tukalime

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Msimu huu tukalime

Mambo ya kukaa mjini tukitegemea wanakijiji waliojichokea ndio watulimie chakula, imepitwa na wakati.

Kila mmoja kama ataamua kulima, vyakula vitashuka bei na maisha yatakuwa marahisi.

Haya mambo yakutafuta hela, na tukitegemea hiyo hela ndio ibadilike iwe chakula; ndicho kinachofanya maisha yanakuwa magumu.

Kwa sababu chakula ni kichache, na wahitaji ni wengi wanaotegemea hela ibadilike ndio iwe chakula.

Tuamke, twendeni tukalime.​
 
Wewe uko wapi mkuu? Huko ulipo kuna mvua ya kutosha?
Maana huku kwetu hata mvua nayo imekuwa ya mgao. Msimu uliopita watu hawakupata mazao ya kutosha na msimu huu nao, mvua ni za kusuasua!
Kutegemea kilimo cha msimu wa mvua ni janga kwa taifa
 
Ni kweli changamoto ni mvua, lakini hata kwa hizi zilizopo ni kujaribu kuzitumia; kwa sababu hakuna mbadala wa chakula.
 
Kilimo nacho Kuna mda ni kama kamari, mwaka mambo yakienda vzr utavuna ila yakikogoma maji utaita mma, mfano mwaka huu mbaazi ilichotufanyia ni majanga nyunyizia sumu lkn mdudu anaendelea kuharibu
 
Kilimo nacho Kuna mda ni kama kamari, mwaka mambo yakienda vzr utavuna ila yakikogoma maji utaita mma, mfano mwaka huu mbaazi ilichotufanyia ni majanga nyunyizia sumu lkn mdudu anaendelea kuharibu
Na hakika unga unaokula umetoka shambani kwako?
 
Hakika! Ila kuna kipindi 2022 nliwahi nunua unga ila sikurudia tena
Kama:-
  • Unga ni wakwako​
  • Mchele ni wakwako​
  • Nyama ya kuku ni ya kwako​
  • Mayai ni ya kwako​
  • Mchicha ni wakwako​
  • Nyanya ni za kwako​
  • Vitunguu ni vya kwako n.k​
Jipigie makofi, wewe ni tajiri.
 
Vingine nanunua maana huu mji hauwezi kuhandle vyote!
Kuna video moja niliona ya mmalawi mmoja, baada ya kuhitimu chuo na kukosa kazi, akaamua kuuza simu yake na kwenda kijijini, ndani ya miaka 3 akawa na mabadiliko makubwa sana, kuanzia kulima mpaka ufugaji, na ameweza pia kuwabadilisha jamii ya hapo kijijini.​
 
Back
Top Bottom