verses fountain
Senior Member
- Sep 30, 2018
- 155
- 195
Habari zenu wakuu JF.
Kwanza kabisa nitoe pole zangu watanzania wenzangu kwa upande wa bara na visiwani na kwa Wote walioguswa na Msiba Wa Raisi wetu John Joseph Pombe Magufuli.
Ni wazi kuna mambo mengi ameyafanya ambayo kwa namna moja ni sawa na anastahili pongezi kwa jinsi Mungu alivyomtumia kutenda hayo mazuri lakini pia kwa kuwa na yeye ni binadamu hawezi kufanya mema peke yake na asikosee.Kwa ukawaida wetu hatupaswi kumsema marehemu vibaya bali kama kuna ambayo alikosea basi kwa wale waliopewa dhamana ya kuchukua nafasi yake wanapaswa kuhakikisha kama makosa yalifanyika basi yasijirudie tena.
Jukumu letu kama watanzania ni kuliombea Taifa letu kuwaombea viongozi walipo madarakani kuanzia ngazi ya chini kabisa mpaka ngazi ya juu Mungu awaongoze kwa hekima na busara wakatimize majukumu yao wakiwa na hofu ya Mungu na wakijua kabisa kwamba kuna leo na kesho na hiyo kesho itakapofika wawe wametimiza majukumu yao kwa nafasi ambayo Mungu amewaruhusu kusimama ili kutenda haki na kuweka usawa katika jamii yetu.
Maombi haya yaelekezwe kwa Uongozi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na mihimili mitatu ya nchi ambayo ni Rais pamoja na baraza la mawaziri, bunge, na mahakama. Wote waliopo katika nafasi hizo wakapate kuhudumia wananchi wakijua kwamba ni kwa neema Mungu amewapa nafasi ya upendeleo wa kusimama pale walipo.
Maombi mengine yaelekezwe kwa nchi yetu kiujumla tukiombea amani, upendo ushikamano, umoja bila kujali tofauti zetu za kidini, kabila, jinsia na chochote kile kisitugawanye watanzania.
Ninaamini kabisa mpaka kufikia kugawanyika kuna vitu vinatumika kugawanya nchi.
Tuombe Mungu atusaidie kisiwepo chochote cha kutugawanya isiwe kwa sasa na hata awamu zijazo.
Tusipende kuwa watu wa kulalamika tu kila siku badala yake tuwe sehemu ya suluhisho kwa kuwaombea Viongozi wetu kwani hakuna binadamu anayeweza kubadilisha moyo wa binadamu mwenzake bali Mungu peke yake.
Watanzania kwa ujumla Tuungane kuliombea taifa letu, viongozi wetu na wananchi wenzetu kwa ujumla.
TUAMKE TULIOMBEE TAIFA LETU,TUNAMHITAJI MUNGU.HATUTAFIKA POPOTE ISIPOKUWA KWA MSAADA WA MUNGU.
Mungu Ibariki Tanzania.