kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Kama tunataka kupambana na machinga tujifunze kupambana na ulanguzi wa bidhaa unaofanywa na wananchi kwa KUSHIRIKIANA na raia wa Kigeni. Serikali inaona machinga wa Kariakoo na maeneo mengine wanakosea kupanga bidhaa barabarani lakini hakuna anayethubutu kukemea kundi la raia wa kigeni lililoibuka hapa nchini linalosambaza bidhaa majumbani Tena kwa mikopo ambayo imefarakanisha familia.
Wapo wageni wengi Sana nchini wenye asili ya kiarabu wanapita majumbani kwetu nakukopesha familia zetu bidhaa. Walifika kwangu Mbeya wakamkuta dada wa kazi wakampa bidhaa za thamani la laki tano na nusu kwa maelezo kwamba atalipa kidogo kidogo. Mimi sikujua, Mara yule dada wa kazi akatoroka na siku anatoroka akaondoka na masufuria aliyokopeshwa na bidhaa nyingine. Siku moja nipo nyumbani weekend wakaja jamaa waliojitambulisha Kama raia wa Misri wakagonga geti la nyumba yangu. Kwa namna walivyokuwa wanagonga nilikasirika kwa sababu kwanza Awana ustaarabu wanagonga Kama walevi. Baada geti likafunguliwa wakanikuta nimevaa pensi na singland, nadhani hawakujua Mimi ndo mwenye nyumba hivyo wakanielekeza nikamwite mwenye nyumba.
Nikauliza wanataka Nini ndipo wakaniambia wamefanya naye biashara na wanamdai laki tano na nusu. Nikashtuka nakumwita mke wangu, alipofika naye akaelewa mchezo ule na hivyo nikapambana nao Kama matapeli. Ndani ya nyumba yangu wale mabwana walitaka kunikunja, sikuwacheka nao nikachukua fimbo nikawalamba stiki wakakimbia nje ya geti na nakupanda geti Kisha wakaondoka. Baadaye baada ya lile tukio ndipo jirani yangu aliponiambia walimkopesha dada wa kazi vyombo.
Baada ya masaa kadhaa wakaja wameambatana na mtu aliyejitambulisha Kama Askari Polisi na kwamba wamekwenda kuripoti kwamba familia yangu imewafanyia fujo walipokuja kudai deni lao. Yaliyoendelea yanafedheesha maana nilikuja kugundua watu Hawa wanafanyabiashara hii kwa baraka za serikali na hii ilitokana na serikali kunilazimisha niwalipe fedha zao japo nilikataa na nikawaambia wamtafute huyo waliyemkopesha. Lakini baada ya kufuatilia nikabaini hawa watu ni wengi mtaani na serikali imewabariki, Sasa kwa mazingira haya tunapambanaje na machinga raia wa Tanzania? Au kwa sababu wao hawana uwezo wakuita dola ikawatetea? Naamini mapambano yakianza na wageni itasadia wananchi kupata ajira nakupunguza machinga barabarani.
Lakini wapo wachina wanaohusika na betting, wamefika kila Kijiji, najiuliza hii kazi ya kukusanya mia mbilimbili inahitaji wachina kweli? Kwamba kampuni ya betting imeajiri wachina kila kata kukusanya miambimbili na sisi tunaamini tutamaliza machinga? Ni sifa zipi zinazopelekea tuwe na wachina wachezesha kamari vijijini? Kwanini wasilazimishwe kuajiri Watanzania na kwanini wasilazimishwe kufanya kazi na mawakala wa pesa mtandao na mabenki kuliko kujaza wachina nchini wanaopunguza chance za Watanzania kuajirowa na kujiajiri?
Kuna wageni wanafanya biashara ten\ rejereja masoko makubwa ikiwemo Karikoo, yaani mgeni anaingiza mzigo kwa mapikauli kutoka China anakuja anafanya udalali na kupata mtaji serikali haipambani naye ili waje watu serious ambao watalazimika kuajiri Watanzania. Sasa hivi kuruhusu wageni wafanye biashara za wazawa na kuwafukuza wazawa kwa sababu tu wamekosa mtaji wakukodi fremu nikuwaonea. Tudhibiti wageni ili Watanzania waaajiriwe kusambaza bidhaa na kutoa huduma zinazofanywa na raia wa kigeni.
Tusipodhibiti na kuwebana wageni nchini kwa sababu tunaogopa mahusiano na mataofa wanayotoka tukaamua kupambana na machinga tunatengeneza bomu la ajira lenye madhara makubwa kuliko kupanga mzigo njiani. Tuache siasa, tuliwaelekeza wapange popote Leo hii tukitaka kuwatoa Basi tuje na mbinu za kuwafanya warasimishe biashara zao kwa kuwatengenezea mfumo. Na njia moja wapo nikuwapeleka kwenye wigo mpana wa kupata bidhaa na kuwaachia wasambaze bidhaa badala yakuruhusu wachina na waarabu waishi soko la machinga.

Upvote
1